jaridahuru

Mitandao

JH STORY: HABIBA UMENIPONZA. --> Kisa cha kusisimua kinachowahusu wanaotarajia kufunga ndoa <--

                            Habiba umeniponza…

“Do not be deceived, bad company corrupts good behavior.” 1 Corinthians 15:33
October 6th, 2012 Siku ya Jumamosi

Ilikuwa Jumamosi…

Kabla sijahamia Kigamboni ninapoishi sasa niliwahi kuishi Tabata. Kabla ya treni la Mwakyembe. Enzi za kugombea daladala na wanafunzi kuanzia wa shule za msingi hadi babu aliyebakiza miezi miwili kustaafu.

Siku hii ilikuwa tofauti kwani Jumamosi huwa hakuna foleni wala kugombania daladala. Niliamka saa kumi na mbili asubuhi na tabasamu kwa mbali nikawaza ratiba ya siku na ilikuwa njema machoni pangu. Nilifanya mazoezi kidogo na kuelekea bafuni kuoga. Kwa kweli moyoni nilikuwa na furaha. Nilioga huku nikiimba kwa ku-hum wimbo wa Stevie Wonder – Isn’t she Lovely.

Nilirudi chumbani na kuvaa t-shirt yangu ya Arsenal (huwa napenda kuvaa jezi yangu ninapojisikia uvivu wa kupasi na kuchagua sana nguo ya kuvaa). Isitoshe baadaye jioni ningepitia mahali niangalie mechi hivyo nitakuwa nimeua ndege wawili kwa jiwe moja na sitohitaji kurudi nyumbani.

Niliwahi kufika ofisini na kwa kweli ile good spirit haikuniacha. Bado niliendelea kutabasamu kwa mbali. Ilipotimia saa sita mchana nilifunga ofisi na kuelekea zangu kutafuta lunch. Nilianza mapema kuwapigia simu marafiki zangu kuwakumbusha kuhudhuria kikao changu cha kwanza cha harusi. Wengi walinihakikishia kuwa wanakumbuka na watafika. Saa nane nilijiondoa maeneo ya Posta kuelekea Usimuache mkeo bar & restaurant kuwasubiri washikaji kwa ajili ya kikao.

Nilikuwa nimemuomba kaka Shabani awe mwenyekiti wa kikao hicho kwani alikuwa tayari amekwisha kuipiga hatua hii ya kuingia kwenye ndoa na alishapitia vikao hivi vya harusi. Nashukuru kwamba alikubali na kwa kweli alikuwa wa kwanza kufika katika kikao. Alikuja na chupa ya Contessa Gin nikamshangaa. Vipi kikao kitaenda kweli? Akaniambia usiwe na wasiwasi mdogo wangu inasaidia kuleta points. Tukaanza kupiga stori pale na baadaye akaja mhudumu, Dorah, kupiga stori na sisi. Kwa jinsi walivyosalimiana na walivyoangaliana kwa kweli nilihisi jambo lakini nikadhani haiwezi kuwa sawa kwani kaka Shabani keshaoa tayari.

Marafiki wengine walifika na kikao kilianza. Siku hii ya kwanza ilikuwa zaidi kufahamiana na kujua nini hasa tunataka kabla ya kukubaliana kuwa tutakapokutana tena tutapanga kamati kwani kila mtu atakuwa ameshajifikiria vyema.

Kabla ya kuondoka pale nilimuona kaka Shabani akiongea na William (mfanyakazi mwenzangu – ambaye naye amekwishaoa) huku wakimuangalia Dorah ambaye kwa kweli alijaaliwa maumbile mema kunako plate number. Wahenga wanasema, yu afaa sana kusafishia kiwi cha macho.

November 10th, 2012 Jumamosi

Jumamosi hii nilikutana na kaka Shabani ila hakukuwa na kikao cha harusi. Tulikutana maeneo yaleyale ya Usimuache mkeo bar. Kama kawaida walikuwa na kaka William na mhudumu wao Dorah ila siku hii alikuwepo mrembo mwingine, Habiba. Habiba ndiye aliyekuwa akileta vinywaji mezani huku Dorah amekaa akipiga stori na sisi.

Katika stori zile ndipo akakumbushia kuhusu mimi kuwa ninatarajia kufunga ndoa mapema mwezi ujao. Wakamwita Habiba na kumuelezea hizo habari. Mwanzoni sikuelewa lengo lao ila niliwasoma hasa baada ya kumlazimisha Habiba akae karibu nami. Tulianza kiutani mwanzoni. Habiba bana alionekana mpole kwa nje hata ukiongea naye kwa mara ya kwanza. Ila ukishamzoea ndipo utayajua makucha yake.

Mtoto wa mjini haswaa nusu Mzaramo nusu Mbondei. Anakuambia amezaliwa anayaona mabasi ya mikoani kila siku utamuambia nini!! Nili-enjoy sana kampani yake kwa kweli. Kidogo kidogo giza likaingia nikawaona Dorah na Kaka William wakielekea kunako counter…hapana waliekea pembeni kwenye ka corridor ambacho baadaye nilikuja kugundua kuna vyumba vya wenyeji.

Nilibaki na Habiba na kaka Shabani tukiendelea na stori. Mara ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yangu. Ulitoka kwa Diana, mchumba wangu. Alikuwa akiniuliza nipo wapi na ningerudi saa ngapi kwani kuna jambo alitaka tuongee. Kwa bahati mbaya wakati nasoma ujumbe ule, kaka Shabani aliuona pia. Akaniambia, “Mdogo wangu huu ndo muda wako wa mwisho kuwa single kabla hujaingia kwenye ndoa. Kwa sasa enjoy muda wako.” Tena akaninong’oneza, “Ka vipi mchukue Habiba hapo one time.”

Sikuyaamini masikio yangu kwani nilitarjia mtu kama yeye anishauri kuwahi kwenda kumsikiliza mchumba wangu, mke wangu mtarajiwa na mama wa watoto wangu. Nililifutilia mbali wazo lile na kumalizia chupa yangu ya Ndovu kwa mafundo makubwa ya haraka haraka na kuwaaga kuelekea nyumbani. Nilishukuru kulishinda jaribu lile na kuapa kuwa sitoingia kabisa katika mkumbo huo wa kutembea na wahudumu wa Bar. Si kwa kuwa si watu, la hasha, ila zaidi sana kwa kuwa tayari nina mchumba na tena ambaye siku za usoni atakuwa mke wangu halali.

November 17th, 2012 Jumamosi

Jumamosi hii nilikuwa nikutane na wenzangu kwenye kikao kingine cha harusi. Kimoyomoyo pia nilitamani sana kuonana tena na Habiba. Alikuwa binti mcheshi na well, kwa kiasi nilitamani kuona wapi ninaweza kufika naye. Lengo langu kubwa ni ku-flirt naye basi!

Kikao kilianza na kama nilivyotarajia, Dorah na Habiba walikuwepo wakihudumia siku ile. Baada ya kikao tulibaki tena na kaka William na Shabani huku wakina Dorah wakija kupiga stori za hapa na pale. Ulianza kama utani kwa Habiba. Mara kikapigwa kibao cha kundi la Little Mix – DNA. Kwanza nilishangaa Habiba kuufahamu wimbo ule na kwamba aliuelewa.

It's the blue in his eyes that helps me see the future
Fingerprints that leave me covered for days, yeah, hey, yeah
Now I don't have any first degree
But I know, what he does to me
No need to work it out, it's so familiar, ooh, ooh, ooh
Mara akaanza kunishika uso kila walipotaja blue eyes na viuchokozi vya hapa na pale na kwa kuwa na mimi niliujua wimbo ule, nikawa naendeleza vitendo sehemu zihusikazo…

It's all about his kiss
Contaminates my lips
Our energy connects
It's simple genetics
I'm the X to his Y
It's the colour of his eyes
He can do no wrong
No, he don't need to try
Made from the best
He passes all the tests
Got my heart beating fast
It's cardiac arrest
He's from a different strain
That science can't explain
I guess that's how he's made
In his d-d-d-DNA
“Aaaah chukueni chumba bana msitutie nyege hapa!” Aliropoka kaka William ambaye tayari Safari na shots za Contessa gin zilikuwa zimeshaanza kumzidi akili. Na mimi kimzaha (ingawa I have to confess nusu ya moyo wangu ulitamani kujaribu ilhali nusu nyingine ilimuwaza mchumba wangu D).
Akilini mwangu niliwaza kuwachokoza nikamuuliza Habiba wapi vyumba vilipo na kama kuna nafasi.

Dorah akadakia kusema, “Vipooooooo” (kwa sauti ya ki-taarab). Nikamnyanyua Habiba na kuelekea kunako vyumba na cha kushangaza alinifuata. Kufika chumbani kwa kweli nilisahau ile nusu ambayo ilitaka kujitunza kwa ajili ya mchumba wangu. Nikajikuta nipo kifuani mwa Habiba. Nusu saa baadaye nikawa nimejilaza kitandani na mawazo tele kichwani huku nikijilaumu kitendo nilichokifanya. Nilingoja hadi kaka Shabani na William walipoondoka ndipo na mimi nikatoka nikalipa bili na kurudi kwangu.

Nilijilaumu kwa muda ila baada ya siku mbili tatu nilisahau na kuendelea na maisha.

November 24th, 2012, Jumamosi

Jumamosi hii tulikuwa tunahitimisha kikao cha harusi na kwamba harusi ingefungwa Jumamosi ya tarehe 8 Desemba. Watu walifika kwa muda ila tuliwakuta kaka William na Shabani wameshaanza kupombeka kwa Govinder Kumar. Kikao kiliendelea vizuri na kumalizika salama. Baada ya kikao kama kawaida (na sasa ilishakuwa tabia) tulikaa na kina Habiba na Dorah kupiga stori. Jumamosi hii Habiba alikuwa mchangamfu kuliko kawaida yake. Nilipata hamu ya kuwa naye karibu na haikutuchukua muda kujikuta watupu chumbani.

Kwangu ile niliichukulia kama bachelor party, last one for the road, na sitorudi tena kwake. Purukushani za mtanange zilianza na baada ya magoli kadhaa pande zote mbili ndipo nilipogundua mechi ile niliicheza bila gloves wala boots. Si kipa wala mchezaji aliyekumbuka kujikinga dhidi ya mashuti ya mwenzake. Nilijipa moyo kuwa kwa kuwa sikuhisi mchubuko wowote basi nitakuwa salama. Na Habiba alionekana mzima kwa kweli…kujipa moyo huku kulikuwa kwa muhimu kwani Jumamosi iliyofuata tulitakiwa kwenda vipimo vya mwisho vya afya mimi na mchumba wangu Diana.

Desemba 1st, 2012 Jumamosi

Adrenaline na ndugu zake wote walikuwa wamepamba moto ndani ya mwili wangu kadri siku ilipokuwa ikikaribia. Niliamka na uchovu kwa mbali ila niliufutilia mbali kwani nilielewa ulitokana sana na hekaheka za maandalizi ya harusi yangu na mrembo Diana. Nilikwenda kujisaidia kwani nilihisi kubanwa sana na mkojo. Nilipofika nilikojoa mkojo wa njano sana nikajiambia moyoni nisipoangalia maandalizi haya ya harusi yatanigharimu afya yangu. Sikutilia maanani sana hata yale maumivu yaliyoambatana na kukojoa.

Niliendelea na ratiba ya siku hadi saa nne alipofika Diana na kunitaka tuelekee wote kwenye vipimo. Tuliingia kwenye gari hao tukaelekea AMREF kwa ajili ya vipimo. Tulipewa ushauri nasaha na msiniulize nilijibuje nilipoulizwa mara ya mwisho kufanya tendo lile. Tulibaki nje huku tukipiga stori za hapa na pale na kupanga vitu vya kufanya katika kumalizia maandalizi.

Kwa kweli marafiki, ndugu na jamaa walikuwa wamejitoa sana kwa ajili ya harusi yetu hivyo michango ilifika kwa wakati na kila kitu kilikwenda kama kilivyopangwa. Nilijihisi tena kwenda kujisaidia na wakati huu maumivu yalizidi kiasi na ile rangi ya njano bado ilikuwepo. Niliwaza kama ni kukosa maji lakini asubuhi ile nilikuwa nimekunywa maji ya kutosha na sikufanya chochote cha kunitoa jasho.

Wasiwasi ulinipata kesho yake baada ya kuendelea kukojoa kwa maumivu nikaamua kumpigia Dr. Chrispin rafiki yangu wa siku nyingi na kumuuliza juu ya suala lile. Aliniambia nifike hospitalini kwake kujua zaidi isijekuwa nimeukwaa. Nilimueleza kuwa jana tu nimetoka kupima na sote mimi na mchumba wangu tulikuwa salama. Ila bado alisisitiza kwenda kwake.

Nilifika na alichukua sample yangu ya mkojo. Tulikaa tukipiga stori na kumueleza jinsi nilivyo na hamu na siku yangu ya harusi. Nilimueleza pia kuwa tumepanga kuelekea Maldives kwa ajili ya fungate letu na pia tulipewa ofa ya kwenda Matema beach tutakaporudi. Kwa kweli hii siku nilikuwa natamani ifike hata kesho.

Leo...November 15th, 2013 Ijumaa

Ni mwaka sasa tangu tukio lile na hadi leo Mentor mimi bado sijaoa. Ilikuja kugundulika kuwa niliambukizwa kisonono na kwa sababu nisizozielewa kilikuwa kimeniathiri sana ndani ya muda mfupi. Ilinibidi kuanza dozi ambayo kutokana na maelezo ya Dr. Chrispin ingenichukua wiki mbili ilhali harusi yangu ilikuwa Jumamosi ya tarehe 8 Desemba 2012.

Ilinibidi kumueleza Diana ukweli wote na ….

Kama Ungependa kujua kilichotokea nilipomueleza Kipenzi Diana ukweli..usione shida kuacha comment hapa chini…

Utamu utamu huishia shubiri…,

Writer:Mentor

Related

JH Story 3441843529180787937

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item