jaridahuru

Mitandao

WAVUVI WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI MGOGORO BAINA YAO NA WAAJIRI WAO!!


ZAIDI ya Wavuvi 1,000 wa Kisiwa cha Kasarazi wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro baina yao na waajiri wao kutokana na kile kinachodaiwa kutoridhishwa na utaratibu wa malipo yao na kutozwa shilingi laki tatu kwaajili ya uwanja na mashine kila wanapoingia ziwani.

Ni kisiwa cha Kasarazi kilichopo katika ziwa Victoria wilayani Sengerema, Kaskazini Magharibi mwa mkoa wa Mwanza, Kisiwa ambacho kimejizolea umaarufu kwa shughuli za uvuvi wa samaki pamoja na dagaa, shughuli hizi za uvuvi zimechangia upatikanaji wa ajira kwa asilimia kubwa ya wakazi waishio pembezoni mwa ziwa Victoria, shughuli ambazo mara nyingi hufanyika nyakati za usiku.

Licha ya uvuvi kuonekana kuwa mkombozi kwa baadhi ya watu kujipatia riziki zao za kila siku lakini bado zipo changamoto zinazowakaibili wavuvi hawa kwa takribani miaka 10, wavuvi wanaona ipo haja ya serikali kuingilia kati mgogoro baina yao na waajiri wao.

Msilikale Juma ni Katibu wa wamiliki wa Vyombo vya Uvuvi katika Kisiwa cha Kasarazi yeye anawatupia lawama baadhi ya wavuvi kutokua waaminifu katika biashara hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela akiwa katika ziara yake wilayani Sengerema anakutana na uongozi huo wa wavuvi pamoja na waajiri wao na hapa anatoa maelekezo juu ya mgogoro huo.
Kisiwa hicho cha kasarazi wilayani Sengerema kina jumla ya wavuvi 1,165 na waajiri wao 50 ampabo hivi karibuni wavuvi hao Kisiwa hicho cha Kasarazi Wilayani Sengerema walistisha kufanya shughuli zao za uvuvi kwa siku nne mfululizo kutokana na mgogoro baina yao na waajiri wao.

Related

Jamii 2364359139359466905

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item