jaridahuru

Mitandao

SOKA: SHAABAN KISIGA AAPA KUTORUDI SIMBA! ASEMA VIONGOZI WA SIMBA WANATAKIWA KUBADILIKA NA KUACHA UDIKTETA


Na Martha Mboma
BAADA ya kuripotiwa kuondoka kambini bila kuwepo kwa taarifa rasmi na kushindwa kuungana na kikosi chake, kiungo mshambuliaji Shaaban Kisiga amefunguka kuwa hana mpango wa kurejea tena Simba.

Kiungo huyo alitimka kwenye kambi ya kikosi hicho mara baada ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City, ambao ulichezwa Jumatano wiki iliyopita ambao timu hiyo ilifungwa mabao 2-1 na hadi sasa ameshindwa kurejea huku uongozi ukijiumauma.
Akizungumza na Championi Jumatano, kiungo huyo alifunguka kuwa, mpira wa hapa Bongo umejaa siasa nyingi, hususan kwa klabu kubwa kama ya Simba, viongozi wanashindwa kushikamana na kuweza kuitengeneza timu na kuwa kitu kimoja.
Kisiga alisema kuwa viongozi wanatakiwa kubadilika si kwa Simba pekee hata timu nyingine endapo tu wanautakia mema mpira wetu.
“Nipo nyumbani kwa sasa na sipo kambini na timu, nipo napumzisha akili yangu lakini Simba sirudi tena kuichezea, ingawa nafahamu kuwa nina mkataba nao, jinsi hali ilivyo kwa sasa siwezi kurejea kule na siwezi kucheza pale.
“Mimi najitambua, nafahamu kitu gani nafanya kwa sababu nimekuwa katika soka kwa muda mrefu, lakini inaonekana siasa zinaumaliza sana mpira wetu.
“Mpira siku zote ni ushindani na kama timu kuanzia viongozi, wachezaji tunatakiwa kuwa kitu kimoja ili kuweza kuwa na mafanikio, lakini Simba imekuwa tofauti kabisa katika suala hilo, kila mtu yuko bize na lake, kweli hapo timu itaweza kufanya vyema kweli?
“Na lawama zimekuwa zikielekezwa kwa wachezaji na makocha pekee, jambo ambalo siyo sahihi,” alisema Kisiga.

Related

Sports 8625968486010012277

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item