JAMII: TAKUKURU YAINGILIA KATI MGOGORO WA ARDHI WA SHULE YA MSINGI WERENI MOSHI

https://jaridahuru.blogspot.com/2015/02/jamii-takukuru-yaingilia-kati-mgogoro.html
Moshi. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imeanzisha uchunguzi wa mikataba ya kubadilishana shamba kati ya Shule ya Msingi Wereni na mfanyabiashara, Thom Ndesamburo.
Mfanyabiashara huyo anayemiliki vitega uchumi kadhaa, aliingia mkataba wa kubadilishana shamba na uongozi wa shule hiyo iliyopo Kata ya Kibosho Magharibi, Wilaya ya Moshi Vijijini.
Thom ni mtoto wa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo anayemiliki Hoteli ya Snow View, vituo vya mafuta na maduka ya kuuza vifaa vya ujenzi.
Taarifa zinadai kuwa, baadhi ya viongozi wa shule hiyo na wale wa Kijiji cha Umbwe Sinde, walifanya udanganyifu katika mkataba huo na hilo limeisukuma Takukuru kufanya uchunguzi.
Habari zinadai kuwa Takukuru inaendelea kuwahoji baadhi ya viongozi wa shule hiyo na viongozi wa Kijiji cha Umbwe.
Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Kilimanjaro, Lawrence Swema alithibitisha kuhojiwa viongozi hao, lakini akakataa kufafanua zaidi kwa madai ya sheria kumzuia kuzungumzia jambo lililo kwenye uchunguzi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Onesmo Kinyaiya alipotafutwa na gazeti hili jana, hakuwa tayari kuzungumza lolote zaidi ya kusema alikuwa ofisi za Takukuru.
Akizungumzia suala hilo, Ndesamburo alisema alifuata taratibu zote na nyaraka husika anazo