JAMII: UKATILI WAENDELEA KUITESA TANZANIA! AMUUA MKEWE KWA KUMCHOMA VISU HUKO TABORA

https://jaridahuru.blogspot.com/2015/01/jamii-ukatili-waendelea-kuitesa.html
Marehemu Zuhura Juma (31) baada ya kuuliwa na mumewe.Na Leah Marco, TABORA/Uwazi
DUNIA inazidi kwenda kubaya! Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Maulid Mussa (35), mkazi wa Kijiji cha Igoko wilayani Uyuwi, Tabora anashikiliwa na jeshi la polisi kwa madai ya kumuua mkewe, Zuhura Juma (31) kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa tisa usiku wa kuamkia Jumatatu ya Januari 12, mwaka huu katika Kijiji cha Usagala Kata ya Magengati Tarafa ya Puge wilayani Nzega, Tabora nyumbani kwa wazazi wa mwanamke huyo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Maulid alifikia uamuzi huo mgumu baada ya mkewe kumuuliza habari alizozisikia kuwa aliuza shamba la tumbaku la familia bila yeye kujua hali ambayo haikumpendeza mwanaume huyo