Saa chache zilizopita katika Barabara ya Kawawa, Ilala Dar imetokea ajali ya moto, gari ndogo imewaka moto lakini hakuna mtu aliyeathirika kutokana na tukio hilo.
Mmiliki wa gari hilo Johns amesema alishtukia watu wakimuita kwamba gari yake inawaka moto kwa sehemu ya chini lakini hajajua kama moto huo kuna sehemu aliukanyaga au ni shoti iliyotoka kwenye gari hiyo.
Kikozi cha Askari wa zimamoto walifika na kuuzima moto huo lakini gari hilo lilikuwa tayari limetekea kwa moto.
Hizi ni picha za tukio hilo.
Watu wakiwa wamelizunguka gari hilo baada ya kuwaka moto.