KITAIFA: UFISADI BANDARI WATIA FORA. MKUTANO MMOJA WATUMIA BILIONI 10
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/11/kitaifa-ufisadi-bandari-watia-fora.html
KAMATI ya Kudumu ya Bunge inayoshughulika na Hesabu za Mashirika ya
Umma (PAC), imemuagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari nchini
(TPA), Joseph Msambichaka, kutoa maelezo ya matumizi ya sh bilioni 20
zilizotumika katika mkutano wa wafanyakazi, matangazo na safari za ndani
na nje za vigogo.
Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe, alimtaka Msambichaka na
Menejimenti ya TPA, kujipanga kutoa majibu sahihi ndani ya wiki mbili
zijazo mjini Dodoma, watakapokuwa wanajadili ripoti ya Mdhibiti na
Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha 2011/12 na
2012/13.
Filikunjombe, alisema kamati yake haiwezi kujadili ripoti ya CAG kwa
siku hiyo kwa kuwa waliipata juzi, hivyo hawajaisoma ili kupata hoja za
kuzifanyia kazi.
Alisema alipopata ripoti ya TPA na kupitia kwa haraka haraka juzi,
alibaini kuna matumizi mabaya ya fedha za walipakodi baada ya kubaini
kuwa, mamlaka hiyo ilitumia sh bilioni 9.6 kwa ajili ya mkutano wa siku
moja kwa wafanyakazi wake.
Alisema fedha zingine zilizotumika kwa matumizi mabaya ni sh bilioni
6.4 zilizotumika kwa ajili ya matangazo na sh bilioni 10 kwa ajili ya
safari za nje na ndani kwa ajili ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo.
“Sasa Mwenyekiti wa bodi TPA, nawataka mkapitie vizuri ripoti hii ya
CAG, baada ya wiki mbili mje na majibu sahihi….Mje mmeshiba chai
kabisa,” alisema Filikunjombe.
Wakati huo huo, siku chache baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Serikali za Mitaa (LAAC) kumtuhumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la
Mwanza, Wilson Kabwe, kusababisha jiji hilo kupata hati chafu na kumtaka
kwenda kujibu hoja, Mkurugenzi huyo amejitetea kuwa aliliacha jiji hilo
likiwa na hati safi.
Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima huku akijibu maswali
kwa ufupi, alisema alipoondoka katika Jiji hilo, aliliacha likiwa na
hati safi na hiyo hati chafu imekuja baada ya kuondoka kwake.
Kuhusu kuhitajika kwenda kujibu tuhuma na hoja kutoka kwa kamati
hiyo, Kabwe alisema hajapata taarifa za kuitwa na isitoshe kama
Mkurugenzi hawajibiki kwa Kamati bali kwa mamlaka iliyomteua.
Kutokana na hilo, alisema endapo atapewa taarifa na wakubwa wake za
kutakiwa kwenda Mwanza, atakwenda kwa sababu yeye ni mfanyakazi wa
Serikali.
Wakihitimisha ziara yao katika Jiji la Mwanza, mmoja wa wajumbe wa
kamati hiyo, Kangi Lugora, alisema ili kuwatendea haki Watanzania na
wakazi wa Mwanza, kamati iliagiza kurudishwa kwa Mkurugenzi huyo kujibu
hoja zilizojitokeza kwenye ripoti ya CAG.
Lugora, alisema cha kusikitisha ni kwamba pamoja na maagizo hayo,
Wizara ya Tamisemi ambayo Wakurugenzi wapo chini yake, imeshindwa
kufanya hivyo na kwa mazingira hayo inashindwa kuwatendea haki
Watanzania ambao ndio walipa kodi wa fedha hizo zinazoliwa na wachache.
Juhudi za kumpata Naibu Waziri wa Tamisemi, Agrey Mwanri, kuzungumzia
sakata hilo, ziligonga mwamba baada ya kupokea simu yake na kudai kuwa
yupo kwenye kikao cha kamati za bunge.
Katika ripoti yake ya Hesabu za kufunga mwaka wa 2012/13 Ofisi ya CAG
ilibainisha kuwa Halmashauri za Jiji la Mwanza, zinaongoza kwa kuwa na
hati chafu.
Halmashauri zinazotajwa kuwa na hati zisizoridhishwa katika Jiji hilo ni pamoja na Halmashauri ya Sengerema, Magu,