jaridahuru

Mitandao

BUNGENI: ULINZI MKALI WAIMARISHWA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE DODOMA, MBWA WA KUNUSA WAONGEZWA




JESHI la Polisi mkoani Dodoma limeendelea kuimarisha ulinzi eneo la kuzunguka jengo la Bunge, licha ya azimio la maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kutotekelezwa juzi.

Kama ilivyokuwa juzi kwa polisi kuifunga barabara ya Dodoma- Dar es Salaam kupitia eneo la Bunge kutotumika kwa magari na watembea kwa miguu, hali hiyo imeendelea kuwa vile vile jana, huku askari wenye farasi, mbwa na silaha wakiendelea kufanya doria kuzunguka jengo hilo.

Wakati ulinzi ukiwa mkali kuzunguka jengo la Bunge, hali ilikuwa tofauti viwanja vya Nyerere Square, ambavyo kwa siku nzima ya juzi vilikuwa chini ya ulinzi mkali wa askari wenye silaha, mbwa na farasi.

Eneo hilo ndiko maandamano hayo yaliyopigwa marufuku juzi, yalitarajiwa kuanzia kuelekea eneo la Bunge. Hatua hiyo ilisababisha shughuli mbambali katika viwanja hivyo vya bustani ya mapumziko kusimama, lakini jana hakukuwa na doria ya askari.

Katika hatua nyingine, wajumbe wanne wa mkutano mkuu CHADEMA, waliokamatwa juzi na kulazwa rumande, waliachiwa jana baada ya kubainika kwamba walikuwa safarini kuelekea Tabora wakitoka jijini Dar es Salaam.

Wajumbe hao ni Christopher Nyamwanji (Mratibu wa kanda ya Magharibi), Laurent Mangweshi (Mwenyekiti wa Mkoa wa Katavi), Elisha Daud na Agness Stephano (wahamasishaji wa kanda ya Magharibi), ambao waliachiwa kwa dhamana jana saa tisa mchana, wakitakiwa kuripoti tena kituoni Jumatatu saa tatu asubuhi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Nyamwanji, alisema kuwa waliondoka Dar es Salaam juzi mchana na kufika Dodoma usiku, ambako walilala ili asubuhi waendelee na safari kuelekea Tabora.
“Sasa kwa utaratibu ulivyo, kiongozi ukiwa kwenye mkoa wowote lazima upite ofisini kujitambulisha, hivyo hata sisi tulipita ofisini kusaini kitabu cha wageni.

“Lakini wakati tupo ndani, kumbe walipita vijana wa chama chetu wakiwa na mabango, wakapanda kwenye gari, kisha wakaondoka bila kuwaona, kumbe kulikuwa na askari aliwapiga picha na kuituma ofisini kwa kamanda akidai tunajiandaa kuandamana,” alisema.

Kwa mujibu wa Nyamwanji, waliondoka ofisini na kuelekea kituo cha mafuta kwa ajili ya kujaza mafuta waanze safari, lakini ghafla walifika polisi na kuwaweka chini ya ulinzi na kupelekwa kituo kikuu cha polisi ambapo waliwekwa ndani hadi jana.

“Walikuja askari tukiwa kituo cha mafuta, wakatukamata wakidai tunataka kuandamana…tulikataa na kujaribu kujitambulisha lakini walituonesha picha za mabango ya wale vijana wakidai ni ya kwetu.

“Hata hivyo baada ya kufikishwa kituoni, gari lilipekuliwa lakini mabango hayo hayakuonekana, isipokuwa kulikuwa na mabegi yetu,” alisema.

Related

Habari Mpya 300482244425812169

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item