VYUONI: WANAFUNZI 100 WAKOSA PA KULALA BAADA YA BWENI LAO KUUNGUA, WADAI CHANZO NI MFUMO WA UMEME
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/08/vyuoni-wanafunzi-100-wakosa-pa-kulala.html
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiWu_ZeQDTUtAQEHA4Zs0swDakkhlUMYbSYex8YFb9ZpX7E1WhpY3tmjl7-hCzcsvvUDEmHJ6rSzjs-Wfzf8HqZfXAsvGDMbAMftbs_nLeVMhkdYn_YOKMM2_ZR8sliyiZC4-1_92Kt1pA/s640/20130711_160542.jpg)
Kilosa. Wanafunzi 100 wa Shule ya Sekondari ya Kilimo ya Kilosa, hawana mahali pa kulala baada ya bweni lao kuteketea kwa moto jana asubuhi.
Mkuu wa shule hiyo, Erasto Luandara alisema moto
huo uliotokea wakati wanafunzi hao wakijiandaa kuingia madarasani
hakijafahamika.
“Mfumo wa umeme katika shule hii umechakaa na mara
ya mwisho ulifanyiwa ukarabati mwaka 2003 na Danida,” alisema mkuu huyo
wa shule.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Elias Tarimo alitembelea
shuleni hapo baada ya tukio hilo na kuwapa pole wanafunzi na uongozi wa
shule kwa tukio hilo.
Tarimo alisema tayari Halmashauri ya Wilaya ya
Kilosa imechukua hatua za kusaidia upatikanaji wa magodoro na madaftari
kwa ajili ya wanafunzi waliokumbwa na mkasa huo.
Mkuu huyo wa wilaya pia alisema amemwagiza
mkurugenzi wa halmashauri kuandaa ripoti kuhusu hali ya shule hiyo
iliyojengwa katika miaka ya 80 kwa msaada wa Serikali ya Cuba, ili
ripoti hiyo iwasilishwe katika ngazi za juu na kufanyiwa kazi.