jaridahuru

Mitandao

KITAIFA: ALIYELIPULIWA NA BOMU LA POLISI MBAGALA AKATWA KIJANJA CHA MKONO, ADAI POLISI WAMFIDIE



Dar es Salaam. Mkazi wa Mbagala Zakhiem, Mwanaharusi Hamis amepoteza kiganja chake cha mkono wa kulia baada ya kulipuliwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu lililorushwa na polisi wakati wakitawanya wananchi.

Mwanaharusi alilipuliwa na bomu hilo Agosti Mosi 2014, saa 3:00 usiku alipokuwa anatoka ndani kwenda msalani.

Akizungumza na gazeti hili jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Wodi ya Mwaisela namba mbili alikolazwa, alisema tukio hilo limebadilisha kabisa mustakabali wa maisha yake.

Mwanaharusi, ambaye ni mama wa watoto wawili alisema alikumbwa na madhila hayo wakati polisi walipokwenda mtaani kwao kumkamata mtuhumiwa wa wizi wa pikipiki. Alisema walipofika, vijana waliokuwa maeneo hayo waliwarushia polisi mawe, ndipo polisi walipofyatua mabomu ya machozi na risasi kuwatanya wananchi hao.

“Ilikuwa saa 3:00 hivi mimi na watoto wangu tukiwa ndani hatujui nini kinachoendelea nje, ghafla tulianza kusikia milio ya risasi na mvumo wa kitu kuelekea upande wa ilipo nyumba yetu. Wakati huo nilikuwa natoka ndani kwenda msalani, nikaona kitu kimenipiga na kunichana sehemu za mkono na miguuni, baadaye nikagundua kilichonipiga kilikuwa bomu,” alisimulia Mwanaharusi.

Alisema baada ya tukio hilo polisi walimpelekea kituoni kwa ajili ya kupata fomu namba ya tatu ya matibabu (PF3) na baadaye Hospitali ya Temeke, alikopewa rufaa ya kwenda Muhimbili kwa kuwa alikuwa akitoka damu nyingi.

“Nimechanganyikiwa. Mimi ndio mtafutaji wa familia, mwanangu wa kwanza amemaliza kidato cha nne na wa pili ana miaka tisa,” alisema.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Temeke, Kienya Kienya alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema ufafanuzi utatolewa leo na kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.

Related

TANZIA : Balozi wa Malawi Nchini Mhe. Flossy Gomile-Chidyaonga amefariki dunia

Aliyekuwa Balozi wa Malawi Nchini Mhe. Flossy Gomile-Chidyaonga alifariki dunia jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi jana. Mhe. Flossy ambaye alikuwa naibu balozi katika ubalozi wa ...

KITAIFA: Meno ya tembo yaibiwa kituo cha Polisi

 Meno ya tembo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya vielelezo mahakamani yalitoweka katika Kituo cha Polisi cha Kilwa mkoani Lindi. Tukio hilo limenukuliwa katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu...

AJALI: Basi la MURO lapinduka

Basi la kampuni ya Princess Muro limeacha njia na kupinduka katika mbuga ya wanyama mikumi. Abiria kadhaa wamejeruhiwa ingawaje bado hakuna taarifa ya kifo iliyotufikia. Taarifa zaidi zitakujia hap...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item