KITAIFA: WAHAMIAJI HARAMU TOKA SOMALIA WAKAMATWA MAKAMBAKO IRINGA WAKIWA NDANI YA ROLI LA SARUJI
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/08/kimataifa-wahamiaji-haramu-toka-somalia.html
IDARA ya Uhamiaji mkoani hapa, imewakamata wahamiaji haramu 21 kutoka nchi ya Ethiopia walioingia nchini kwa kutumia roli la kubebea saruji katika eneo Mashujaa mjini Makambako.
Naibu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji, Rose Mhagama alisema wahamiaji hao walikamatwa Agosti 14, mwaka huu, saa 12:30 jioni wakati kikosi cha uhamiaji kikiwa katika doria.
Mhagama alisema kuwa kikosi hicho kilifanikiwa kubaini lori lililowabeba likitokea Makambako kuelekea Songea lenye namba za usajili T587 CSN likiwa na tela namba T780 CHM lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la Nyange.
Alisema lori hilo ni mali ya Everest Flight LTD, ambapo baada ya dereva huyo kukaguliwa alieleza kuwa alikuwa akiwasafirisha kuelekea nchini Malawi.
“Dereva alipohojiwa alisema alikuwa anakwenda kukutana na mtu ambaye anahusika na watu hao akiwa mjini Njombe, ili aweze kuwashusha pale Njombe na waweze kuendelea na utaratibu wao wa kwenda Malawi,”alisema.
Mhagama alieleza kuwa jeshi la polisi linamsaka dereva huyo baada ya kutoroka na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kuwafichua wahamiaji haramu.