KIMATAIFA: SERIKALI YA LIBERIA YAANZA KUWATAFUTA WAGONJWA WA EBOLA WALIOTOROKA KAMBINI
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/08/kimataifa-serikali-ya-liberia-yaanza.html
Kituo kilichotengwa na kuwekewa karantini kwa sababu
ya ebola, kimeshambuliwa na zana kuporwa katika mji mkuu wa Liberia,
Monrovia.
Washambuliaji walipora magodoro na vitu vyengine.
Mwandishi wa BBC katika kanda hiyo anasema pengine washambuliaji walikerwa kuwa kituo hicho kimewekwa katika mtaa wao.
Wakuu wa Liberia wanajaribu kuwatafuta wagonjwa waliotoroka ili kuwarejesha tena kwenye kituo hicho.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi.