KIMATAIFA: VIKOSI VYA MAREKANI VYAZIDI KUISHAMBULIA IRAQ, RAISI AJIONGEZEA MUDA YAGEUKA VITA NA WAZIRI MKUU
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/08/kimataifa-vikosi-vya-marekani-vyazidi.html
Marekani imeendeleza mashambulizi ya anga kaskazini
mwa Iraq kwa lengo la kuwasaidia Wakrud katika mji wa Erbil dhidi ya
wapiganaji wa kiislam wa kundi la Jihad.
Wapiganaji wa kundi hilo la Kiislam hivi
karibuni wameendelea kuimarisha ngome yao katika eneo hilo ikiwa ni
pamoja na kuiteka ngome kubwa ya Iraq katika mji wa Mosul.
Jeshi la Marekani limesema limefanya
mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Sunni waliokuwa wamejificha katika
milima iliyo eneo la wakimbizi la Yazid.
Hata hivyo Uingereza imesema inaendelea kutoa
misaada ya kibinadamu kwa Wakurdi ambapo Ofisa wa zamani wa mambo ya
kigeni wa Uingereza Alistair Burt anasema nchi hiyo inaweza kusaidia
eshi la Wakurdi.
Wakati huo huo vikosi vya majeshi ya Iraq na
vyombo vya usalama vimesambaa katika katika maeneo mbalimbali ya mji wa
Baghdad huku kukiwa na hali ya wasiwasi kufuatia kauli iliyotolewa na
waziri mkuu wa nchi hiyo ya Iraq Nouri al-Maliki inayodaiwa kuwa ni ya
utovu wa nidhamu kwa Rais wa nchi hiyo Fuad Masum.
Amesema kuwa Rais wa Jamhuri hiyo amevunja
katiba mara mbili,mara ya kwanza ni pale alipojiongezea muda wa kukaa
madarakani,wakati alistahili kutangaza kuvunja bunge. Hata hivyo kipindi
chake kiliisha august saba alhamisi iliyopopita.
Hata hivyo papa Francis ameelezea gogoro wa Ira
kwamba msingi wake mkubwa ni masuala ya tofauti za kidini. Melfu ya watu
nchini Iraq wamekuwa wakilazimishwa na wapiganaji wa kiislam ambao
wameimarisha ngome ao kaskazini mwa nchi hiyo.Katika ujumbe wake wa
jumapili ,papa Francis ametoa wito kwa dunia kukomesha uhalifu huo
unaoendelea nchini Iraq.