jaridahuru

Mitandao

TAHADHARI: JIEPUSHE NA KAMPUNI HII YA YA KITAPELI, INADAI KUWA INATOA MIKOPO BILA RIBA



SOCIAL Company inayojinasibu kutoa mikopo nafuu isiyokuwa na riba kupitia mfuko wake maalum ujulikanao kama Social Credit & Loans, imegundulika kuwa ya kitapeli.

Kampuni hiyo imekuwa ikitumia majina ya watu maarufu kama vile Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda na mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ikielezwa kwamba ni miongoni mwa wale waliofaidika na mikopo hiyo.

Kwa nyakati tofauti wawili hao walikana kuwa miongoni mwa watu waliowahi kufaidika au kuomba mkopo kutoka kwenye kampuni hiyo.

Kampuni hiyo ambayo tayari imewatapeli watu mbalimbali nchini, imekuwa ikizama zaidi kufanya utapeli huo kwa kutumia njia ya mtandao ambako huwataka wateja wao kujiunga kwa kupitia tovuti.
Katika ukurasa wa tovuti ya kampuni hiyo, wateja kabla ya kujisajili hutakiwa kutoa kwanza sh.
84,000 kama ada ya ushirika ambayo inatakiwa kuingizwa kwenye akaunti ya M-Pesa na TIGO-Pesa ili waweze kuwa na sifa ya kukopeshwa fedha kuanzia sh. 200,000 hadi 10,000,000 kwa muda wa dakika 45 baada ya kujiandikisha.

Wanaelezea kwamba baada ya mteja kujaza fomu hiyo na kulipia ada yake, fomu yake itapokelewa na bodi kuu ya utoaji mikopo, pia malipo yake yatapokelewa na mhasibu na baada ya hapo maombi yake yataidhinishwa na atapatiwa mkopo wake usiokuwa na riba.

Kwamba sababu za kutoa mikopo bila riba kwa kupitia mfuko wao maalum wa Social Credit & Loans inachangiwa na faida wanazozipata kutoka kwenye kampuni za simu pindi mteja anapojaza fomu na kulipia ada kwa njia ya mitandao hiyo.

Kampuni hiyo inayoonyesha kwamba imepata usajili kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kupewa TIN namba 203-334-6789 ikiwa na usajili namba TRA. 33/SCC/REG.7894, imeanzishwa tangu mwaka 2003 ikiwa kama tawi zawa lisilojitegemea na ni kampuni binafsi iliyoingia ubia na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa makubaliano ya mikataba ya muda.

Imeeleza kuwa baada ya Social Credit Company kumaliza mkataba wake rasmi na NBC, kwa sasa wameanza kujitegemea na kuunda mfuko huo wa Social Credit & Loans kwa ajili ya kutoa mikopo.
Tanzania Daima lilifika katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo eneo la Kigamboni, Mji Mwema, lakini mlinzi wa jengo hilo alisema kuwa wamiliki wa ofisi hiyo hawafiki mara kwa mara.

Msemaji wa Vodacom, Salum Mwalimu, alikana kampuni yao kujihusisha na utoaji wa mikopo.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alikana kampuni hiyo kutambuliwa.

Kayombo alisema kuwa amejiridhisha baada ya kuifuatilia kampuni hiyo katika mfumo wa kompyuta wa TRA, na kwamba wameshindwa kuitambua namba iliyotajwa kwenye fomu F-TSD 002-B.

Aliongeza kuwa wamegundua kwamba kuna tatizo katika mfumo wa TIN wa TRA unaoruhusu tarakimu tisa, wakati ile iliyotumika katika kampuni hiyo ina tarakimu kumi na pia ameshindwa kumtambua mhusika anayetumia jina la ‘Social Company’.

Related

Jamii 7044179934314727714

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item