jaridahuru

Mitandao

KITAIFA: WAZIRI WA MALIASILI AGEUKWA, KAMPUNI YA UWINDAJI KUMFIKISHA MAHAKAMANI KWA TUHUMA NZITO MALIASILI

 



UONGOZI wa Kampuni ya Uwindaji wa Kitalii ya Green Mile Safari Ltd (GMS), umesema haukubaliani na uamuzi wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wa kuwafutia leseni, hivyo wameahidi kulifikisha suala hilo mahakamani.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mtanzania Awadh Ally Abdallah, Wakili Alloyce Komba alisema upo mgogoro wa kimaslahi kati ya GMS na kampuni ya Wengert Windrose Safaris Ltd (WWS) iliyokuwa ikimiliki kitalu cha Lake Natron Game Controlled Area (East) kwa miaka 15.

Wakili huyo wa kujitegemea alisema baada ya GMS kushinda zabuni mbili za uwindaji katika kitalu hicho na kingine cha Eneo la Pori la Akiba la Selous kiitwacho MK1 kwa msimu wa 2013/2018, kampuni ya WWS ilitaka kuuziwa kitalu cha Lake Natron jambo.

“Wakati huo WWS hawakuwa na sifa za kuendelea kuwinda eneo hilo walipoona GMS imepata leseni wakaja kuomba tuwauzie kitalu, tulikataa badala yake tulikubali kuwauzia safari za kitalii sio kitalu.

“WWS ni kampuni tanzu ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ya nchini Marekani…zikaibuka tuhuma kwamba wizara imewanyang’anya kitalu, ni tuhuma za kutungwa na zilifikishwa hadi Ikulu ya Marekani muda mfupi kabla Rais Obama hajafika Tanznaia.

“Nataka watanzania wote wajue kwamba lengo la tuhuma hizo ni kutaka serikali ya Tanzania imnyang’anye kitalu hicho GMS ambayo wakurugenzi wake ni Abdallah na Sheikh Abdulla Hamed bin Butti Alhamed raia wa Uarabuni,” alisema wakili Komba.

Kwa mujibu wa wakili huyo, waziri Nyalandu anatumika vibaya na Wamarekani kumkandamiza mwekezaji mzawa kwa maslahi binafsi huku akitilia shaka safari yake ya Marekani muda mfupi baada ya kutangaza kuifutia leseni GMS huku akisisitiza kwamba ni shinikizo kutoka kwa Wamarekani.

Alisema kampuni hiyo imekopa na kuwekeza mtaji wa dola milioni 10 za Marekani kutoka moja ya benki kubwa huko Uarabuni, deni litakaloanza kulipwa baada ya miaka mitano hivyo kufungia leseni zao ni kuwahujumu.

Wakili huyo pia alisema mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji, Peter Msigwa yupo nyuma ya uonevu huo huku akibainisha kwamba picha alizozionyesha mbele ya waandishi wa habari ni baadhi ya video iliyochukuliwa na GMS wakati wa ziara ya mwana mfalme wa Uarabuni.

Komba alikanusha kwamba aina ya uwindaji uliofanywa ulikiuka sheria na kubainisha kuwa picha zilizotumiwa na mchungaji Msigwa zilitumika kwa nia ovu.

Mchungaji Msigwa ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, aliwaonesha waandishi wa habari namna kampuni ya GMS ilivyokiuka sheria za uwindaji kwa kutesa wanyamapori alipokutana nao Julai 4 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Msigwa, GMS ilifanya uwindaji wa kukiuka sheria katika kitalu cha Gonabis/Kidunda- WMA na kitalu cha MKI- Selous, katika kipindi cha uwindaji cha mwaka 2012.
Licha ya kukanusha tuhuma hizo, wakili Komba alieleza namna WWS inavyowabugudhi wageni wanaofika kwenye kitalu hicho ikiwemo kuchimba mashimo kwenye uwanja mdogo wa ndege ili kuzuia wageni wasifike eneo hilo na kwamba ni mwaka wa pili sasa GMS haijafanya biashara iliyokusudiwa kutokana na kero hizo.

“Tunashindwa kufanyabiashara kule kila kukicha ni vurugu za WWS hadi Julai 19 mwaka jana, Mkuu wa Wilaya ya Longido aliwaonya wenzetu kwa vitendo vyao vya kuchochea wananchi wafanye vurugu,” alisema.

Katika maelezo yake, muda mwingi alisisitiza kwamba waziri Nyalandu anatumika huku akibainisha kwamba si mwadilifu kwa kukubali kutumika na Wamarekani na kwamba mahali pekee pa kupata haki iwapo mamlaka za juu zitashindwa nimahakamani.

Chanzo: Magazeti | Tanzania Daima

Related

Kitaifa 2264447714540554237

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item