jaridahuru

Mitandao

SOKA: WACHEZA 6 WA TIMU YA SHAKHTAR DONETSK WAGOMA KURUDI KIKOSINI, WADAI BADO UKRAINE KUNA VITA




WACHEZAJI 6 wa Shakhtar Donetsk wamekataa kurudi Mji wa Donetsk huko Ukraine kutokana na Vita ya wenyewe kwa wenyewe Nchini humo.

Mji wa Donetsk uko kwenye eneo linalomilikiwa na Waasi wanaoungwa mkono na Urusi huku Jeshi la Ukraine likipigana kutaka kulikomboa.

Klabu ya Shakhtar Donetsk ilikuwa huko France Wikiendi iliyopita kucheza Mechi ya Kirafiki na Lyon lakini Wachezaji Alex Teixeira, Fred, Dentinho, Douglas Costa, Facundo Ferreyra na Ismaily waligoma kurudi Ukraine.

Rais wa Klabu hiyo ambae pia ndie Mmiliki wake, Rinat Akhmetov, amewaonya Wachezaji hao kwamba wataadhibiwa vikali.

Amesema: “Wachezaji wana Mikataba ambayo inabidi waiheshimu. Kama hawarudi wao ndio watakuwa wa kwanza kuumia.”

Nae Meneja wa Shakhtar anaetoka Romania, Mircea Lucescu, amemlaumu Wakala wa baadhi ya Wachezaji hao, Kia Joorabchian, kwa kuwashawishi kugoma kurudi Ukraine.

Meneja huyo amedai Wakala huyo anataka kutumia machafuko ya Ukraine anufaike kwa kuwafanya Wachezaji hao kuwa huru wakati wana Mikataba.

Watano kati ya Wachezaji 6 waliogoma kurudi ni kutoka Brazil na Ferreyra ni Mtu wa Argentina.
Hivi sasa Shakhtar hawaruhusiwi kuutumia Uwanja wao wa Nyumbani, Donbass Arena uliopo Mjini Donetsk, kutokana na Vita hiyo lakini, huku Msimu mpya ukitakiwa kuanza Wikiendi hii, Shirikisho la Soka la Ukraine halijaamua Klabi hiyo itacheza wapi Mechi zake za Nyumbani.

Related

MICHEZO: TAIFA STARS YATOA SULUHU YA 2 - 2 NA BLACK MAMBAS YA MSUMBIJI, KHANIS MCHA APACHIKA YOTE 2

 Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Msumbiji katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam....

WC 2014: RAISI WA FIFA NA MARADONA WAIPONDA TUZO ALIYOPEWA, WASEMA HAKUSTAHILI TUZO HIYO

  Rais wa Fifa Sepp Blatter amesema ameshangazwa kuwa Lionel Messi alishinda tuzo ya mchezaji bora - Golden Ball Award- katika Kombe la Dunia. Messi, 27, alitajwa kuwa mchezaji bora...

WC 2014: UJERUMANI YALAMBISHA JOKER BRAZIL, YATANDIKA 7-1 NA KUTINGA FAINALI, SIRI NZITO YAFICHUKA BAADA YA MECHI

UJERUMANI imetinga Fainali ya Kombe la Dunia, baada ya kuwafumua wenyeji, Brazil mabao 7-1 katika mcheo wa Nusu Fainali uliofanyika Uwanja wa Mineirao mjini Belo Horizonte, Brazil. Ujerumani ina...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item