KIMATAIFA: TAHADHARI YA MASHAMBULIZI NCHINI UGANDA, POLISI WATANDA MJI WA KAMPALA

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/07/kimataifa-tahadhari-ya-mashambulizi.html
Polisi nchini Uganda wamedhibiti usalama mjini
Kampala kufuatia onyo la mashambulizi ya kigaidi kupangwa kufanywa
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe.
Kundi la wanamgambo la Al shabaab lilishambulia mikahawa miwili mjini Kampala mwaka 2010 wakati wa fainali ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini.
Zaidi ya watu 70 waliuawa katika mashambulizi hayo, wakati ambapo washambuliaji wa kujitoa manga walipojilipua wakati mashabiki wa soka walikuwa wakitazama michuano hiyo.
"kulingana na taarifa za ujasusi, kuna tisho maalum dhidi ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe na kundi la kigaidi lisilojulikana. Tisho hilo haliwezi kuchukuliwa kwa wepesi, '' ilisema taarifa ya maafisa wa usalama.
Taarifa hiyo ilisema kuwa shambulizi lilipangwa kufanywa kati ya saa kumi na mbili jioni na saa mbili usiku.
Vikosi vya usalama vimeweka vizuizi katika uwanja huo na katika baadhi ya barabara zilizo umbali wa kilomita 32 kutoka uwanja huo.
Mikutano kadhaa ya kimataifa inafanyika nchini humo na lengo la maafisa wa usalama ilikuw akuwahakikishia usalama wao wajumbe wanaohudhuria mikutano hiyo