jaridahuru

Mitandao

JAMII: MZINDAKAYA AONJA CHUNGU YA MAGUFULI, ANYANG'ANYWA NYUMBA 12 NA WIZARA YA UJENZI

WIZARA ya Ujenzi imeinyang’anya Kampuni ya Agriculture and Animal Food Industries Ltd (Saafi), inayomilikiwa na mwekezaji mzalendo na mwanasiasa mkongwe, Dk. Chrisant Mzindakaya nyumba 12 za umma ambazo ilikuwa imezipanga kibiashara kwa miaka 12.

Nyumba hizo 11 za kuishi na moja ofisi zilizojengwa na Shirika la Maendeleo la Norway mwaka 1988,  zimekabidhiwa rasmi Juni 17 mwaka huu, kwa Wakala wa Majengo (TBA), mkoani hapa na Wizara ya Ujenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi huo wa serikali baada ya kukagua nyumba hizo juzi, Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly (CCM), alisema ana furaha kwani nyumba hizo zilikuwa zikimnyima usingizi kutokana na maofisa serikalini wakiwemo majaji na baadhi ya wakuu wa idara kuishi nyumba za kupanga, lakini sasa wataishi nyumba hizo ambazo ni bora na zenye usalama wa kutosha.

Alibainisha kuwa baada ya kutembelea nyumba hizo na kuzikagua akiongozana na Meneja wa Wakala wa Majengo Mkoa wa Rukwa, Deocles Kalikawe, amebaini kuwepo kwa upungufu mkubwa ambao alidai mwekezaji aliyezipanga kibiashara atalipia gharama zote za ukarabati.

“Nampongeza Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kwa uamuzi mgumu aliofanya wa kuzirejesha  nyumba hizi serikalini kupitia TBA… Nimemshauri Meneja wa TBA mkoani hapa, moja ya nyumba hizi iwe kwa ajili ya kufikia viongozi wa kitaifa, kwani iliwahi kutokea tulifikiwa na wageni wawili kutoka taifani, mmoja alilala Ikulu ndogo, lakini mwingine alilazimika kulala hotelini,” alisema.

Meneja wa TBA mkoani hapa, Kalikawe, alieleza kuwa mara baada ya kukabidhiwa rasmi nyumba  hizo, waliamua kuweka walinzi wao wakati wakijipanga kufanya tathmini ya ukarabati ili ziweze  kupangishwa kwa majaji, watumishi wa mahakama na wakuu wa idara.

Baadhi ya wakazi wa mjini hapa waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi, wameipongeza serikali kwa kuchukua uamuzi huo na kwamba utapunguza tatizo la uhaba wa nyumba.

“Tatizo la uhaba wa nyumba ni changamoto kubwa sana mkoani hapa… imesababisha baadhi ya watumishi wanaopangiwa kuja kufanya kazi huku kukataa kuripoti au wanafika lakini wakiondoka  hawarudi tena,” alisema Enos Budodi, mkazi wa mjini hapa.

Mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na shughuli za kijamii na maendeleo (Udeso) kwa mikoa ya Rukwa na Katavi, Eden Wayimba, alisema uamuzi wa serikali kujireshea mali yake, utawapunguzia gharama za maisha watumishi wa umma watakaopangishwa.

Kurejeshwa kwa nyumba hizo ni ushindi kwa Aeshi, ambaye tangu awali amekuwa hana uhusiano mzuri wa kisiasa na Dk. Mzindakaya, ambapo mara kadhaa alikuwa akihoji uhalali ya nyumba hizo kumilikiwa na kampuni ya mtu binafsi badala ya kutumiwa na watumishi wa serikali.

Lakini wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanadai uamuzi huo utaongeza chuki ya kisiasa kati ya wanasiasa hao wawili ambao mara ya mwisho walikutana Mei mwaka huu kwenye ibada ya kusimikwa kwa Askofu wa Kanisa la Moravian, Jimbo la Rukwa, Cornad Nguvumali.

Ibada hiyo, ilifanyika kwenye uwanja wa michezo wa Nelson Mandela mjini hapa, ambapo mkuu wa mkoa aliwataka wazike tofauti zao, lakini Dk. Mzindakaya alikataa kumsamehe Aeshi kwa madai hakuandaliwa kiroho kutoa msamaha kwenye ibada hiyo

Related

Jamii 3351017352781090304

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item