jaridahuru

Mitandao

BURUDANI: BAADA YA KURUDI KA KISHINDO KWENYE 'GAME' ALIKIBA APANGA KUZINDUA NYIMBO 2 KWENYE TAMASHA LA MATUMAINI



MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba ‘Alikiba’, anatarajia kulitumia Tamasha la Matumaini 2014 kuzindua rasmi nyimbo zake mbili zinazotikisa anga la Bongo Flava kwa sasa za ‘Mwana’ na ‘Kimasomaso’, huku akikiri kufarahishwa na mapokezi ya singo hizo kwa mashabiki nchini.
 
Tasnia ya muziki huo nchini kwa sasa imegubikwa na gumzo la kazi hizo mbili za Alikiba, , alizofanyia katika studio mbili tofauti za Combination Sound chini ya mtayarishaji mahiri Man Walter na MJ Records chini ya Marco Chali.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Tanzania Daima, Alikiba alisema kuwa Tamasha la Matumaini lina maana kubwa kwake na kila Mtanzania, hivyo ameamua kulitumia kuzindulia nyimbo hizo, zilizomrejesha kwa kasi baada ya kimya kirefu kilichotokana na harakati tofauti.

“Tamasha la Matumaini, kama jina lake lilivyo ni maalum kurejesha matumamini kwa waliopoteza. Niliwahi kupoteza matumaini ya harakati zangu huko nyuma wakati naanza tasnia hii, lakini kupitia kitu kama hiki, nikaweza kusimama na kuwa Alikiba mwenye jina na mafanikio niliyonayo sasa,” alisema mkali huyo.


Aliongeza kuwa kwa kutambua hilo amewataka Watanzania kumiminika kwa wingi Uwanja wa Taifa Agosti 8, kushuhudia shoo kali atakayofanya sanjari na nyota wengine wa muziki huo watakaotumbuiza katika tamasha hilo, ambalo litawarejeshea matumaini katika nyanja na tasnia tofauti walizomo.

Alisema baada ya tamasha, ataanza rasmi mchakato wa kuandaa video ya vibao hivyo, alivyovitaja kuwa ni zawadi maalum kwa mashabiki wake, ambao walimpa wakati mgumu akitafakari namna ya kutii kiu.

“Kimya kingi kina mshindo mkuu kaka. Nilibanwa na masuala mbalimbali, kama vile michakato ya kibiashara, mapumziko maalum yaliyotokana na kufululiza muziki kwa muda mrefu na pia kumpaisha bwana mdogo (Abdul Kiba). Sasa niko kamili, hakuna kulala wala kupumzika tena, ni ‘non-stop’ kwa kwenda mbele,” alisema Alikiba.

Related

MICHEZO: MANYIKA HARUDI SINGIDA UNITED NG'OO (BABA WA MANYIKA)

BABA mzazi na Meneja wa kipa wa Singida United, Peter Manyika, Manyika Peter amesema kuwa mwanawe hawezi kurudi katika timu hiyo licha ya viongozi wake kusema wanajipanga kumrudisha. Hivi karibuni ...

BURUDANI: JE!? UNAFAHAMU KUWA A.Y NDIYE MMILIKI WA KIPINDI CHA MIKASI - EATV NA SALAMA JABIR?

Tasnia ya sanaa hususan muziki ni kazi kama ilivyo kwa fani nyingine na endapo walioamua kuichagua watakuwa na bidii, inaweza kuwainulia kipato na kujikuta katika maisha bora. ‘AY’ au Mzee wa Commer...

SOKA: MBEYA CITY YAMGEUZIA KIBAO JOHN BOCCO

Dar es Salaam. Klabu ya Mbeya City imewasilisha taarifa ya rufaa kwenda Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikieleza upungufu mwingi na kutaka wachezaji wa Azam wachukuliwe hatua za kinidhamu. Kati...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item