jaridahuru

Mitandao

BUNGENI: LAWAMA ZAWAGEUKIA ROSE MIGIRO, SITTA NA NAIBU WAKE KATIKABUNGE LA KATIBA




MTETEZI wa haki za wanawake, Ananilea Nkya, amesema kuvurugika kwa Bunge Maalum la Katiba, wa kulaumiwa ni Mwenyekiti Samuel Sitta, Makamu wake Samia Suluhu na Waziri wa Katiba na Sheria, Asha Rose Migiro.

Akizungumza juzi katika kipindi cha ‘Kipima joto’ kinachorushwa na runinga ya ITV, Nkya, alisema kuwa hakuna sababu ya kumtafuta mchawi wa kushindwa kupatikana katiba mpya kwani viongozi hao ndio chanzo cha mparaganyiko.

Alisema kuwa viongozi hao walipaswa kusimamia rasimu ya katiba na si kuchukua maoni ya Rais Jakaya Kikwete, kwani hana kosa kutokana na hotuba.

“Kilichokuwa kinajadiliwa ni rasimu ya pili ya katiba ambayo Rais Kikwete aliisaini baada ya kukamilika maoni ya wananchi, na wao kama viongozi wa Bunge hawakutakiwa kufuata ya rais bali ya rasimu ya katiba,” alisema.

Alisema kuwa Sitta alipaswa asimamie rasimu yenye maoni ya wananchi, lakini walichofanya yeye na viongozi wenzake ni dhahiri wameshindwa kwakuwa wamedharau kile wananchi walichopendekeza.

Related

Habari Mpya 5159222312386025156

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item