jaridahuru

Mitandao

SIASA: NEC YAKIRI KUWEPO KWA KASORO NYINGI KATIKA DAFTARI YA WAPIGA KURA


Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema daftari la kudumu la wapiga kura lililopo limegubikwa na kasoro nyingi zinazowafanya watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa kuinyooshea kidole tume hiyo.


Akizungumza na viongozi wa dini jijini hapa jana, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva, alisema tume hiyo imeanzisha mchakato wa kuboresha daftari hilo kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voter Registration (BVR), ili kuondoa hofu iliyopo.


Mwenyekiti huyo alisema kuwa ni ukweli ulio dhahiri kwamba teknolojia ya Optical Mark Recognation (OMR) iliyotumika katika uchaguzi uliopita ilisababisha kasoro kwenye daftari la kudumu la wapiga kura hatua iliyosababisha wadau wa uchaguzi kuhoji uhalali wake.


Alisema ameamua kuongea na viongozi hao wa dini ili wakawaambie waumini wao kuwa zoezi hilo la usajili litakalochukua siku 14 litaanza hivi karibuni.


“Vifaa kwa ajili ya zoezi hilo vimekwisha agizwa na Tume itavipokea Agosti, 2014 ili kuanza zoezi hilo.


Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa dini walihoji uamuzi wa NEC kuwaomba kwenda kuwaambia waumini wao kwenye maeneo ya ibada wakati wamekuwa wakizuiwa kuzungumzia masuala ya siasa katika maeneo hayo.


Sheikh Mussa Kundecha kutoka Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi ya Kiislamu, aliitaka NEC kueleza namna viongozi hao mpaka uliopo baina ya dini na siasa: “Mmekuwa mkiwazuia viongozi wa dini na siasa na mimi najua jambo hili halitaishia kwenye kujiandikisha tu, litakwenda hadi kwenye uchaguzi, sasa tunatofautishaje na siasa?”


Akijibu swali hilo, Jaji Lubuva alisema: “ Tatizo linakuwa pale unapowaambia waumini wakipigie kura chama fulani kwa sababu kimeletwa na Mwenyezi Mungu.

Related

Siasa 6189423830323336109

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item