BURUDANI: WEMA SEPETU APATA UJAUZITO, DIAMOND PLUTNUMZ APAGAWA
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/burudani-wema-sepetu-apata-ujauzito.html
‘Beautiful Onyinye’ na kipenzi cha Diamond, Wema Sepetu sasa ni mjamzito. Baada ya misukosuko ya muda mrefu ikiwemo kuporwa na wasichana wenzake penzi lake la Diamond, sasa Wema amepata kile alichokuwa akikililia kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, inadaiwa kuwa Diamond kwa sasa kawa kama mtu aliyepagawa kwa furaha kutokana na taarifa hizo njema na tayari ameshaanza maandalizi ya kijacho chake….
Kugundulika kwa ujauzito wa Wema ni baada ya kuanza kujisikia vibaya walipokuwa Afrika Kusini ikiwemo kichefuchefu na kizunguzungu alipokuwa hotelini alipofikia na kulazimika kwenda hospitali kwa uchunguzi zaidi,
Inasemekana kuwa Wema alisindikizwa na Aunt Ezekiel kwenda hospitalini waliyekuwa naye huko Afrika Kusini kumpa sapoti Diamond na madaktari ndiyo waliomjuza kuwa anakiumbe tumboni cha wiki 7.
Taarifa za madaktari hao zilimfanya Wema awe kama mwehu
aliyepagawa na kurudi hotelini kwa mumewe Diamond huku akiwa
na tabasamu ambalo hapo awali Diamond hakuwahi kuliona….
Inasemekana kuwa mpaka sasa siyo Diamond wala Wema
aliyewaambia wazazi wake kuhusiana na mimba hiyo zaidi ya
watu wa karibu wa wawili hao waliowasindikiza Afrika Kusini.


