https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/michezo-seedorf-aoneshwa-mlango-wa.html
AC Milan wamemfukuza kazi Kocha Clarence Seedorf na kumpa kazi hiyo Filippo Inzaghi.
Seedorf
amefukuzwa kazi ikiwa ni pungufu ya miezi mitano tu tangu achaguliwe
kushika nafasi hiyo kwa klabu inayocheza Ligi Kuu ya Italia – Serie A.
Mdachi huyu mwenye umri wa miaka 37 alipewa mikoba kwenye klabu aliyochezea kwa miaka 10 tangu 2002.
Inzaghi
naye ni mkongwe aliyechezea AC Milan lakini hajapata kufundisha timu
iliyo katika ligi kuu. Alikuwa akifundisha timu ya vijana chini ya miaka
19 y AC Milan.(P.T)
Inzaghi
(40) amepewa mkataba wa miaka miwili na ameajiriwa baada ya mmiliki wa
klabu na rais wake, Silvio Berlusconi kusema Ijumaa iliyopita kwamba
Seerdof ni sehemu ya walioshindwa kazi hapo San Siro. Berlusconi ni
waziri mkuu wa zamani wa Italia na ni mfanyabiashara bilionea
anayemiliki pia vyombo vya habari.
Enzi za
kusakata kwake soka, Inzaghi alichangia kwa kiasi kikubwa Timu ya taifa
ya Italia kutwa ubingwa wa dunia 2006, makombe mawili ya Uefa na makombe
matatu kwa AC Milan katika Serie A.
Seedorf
alichukua nafasi ya kocha aliyemtangulia, Massimiliano Allegri
aliyefukuzwa kazi kutokana na kuanza vibaya msimu wa Ligi Kuu 2013/14.
Aliajiriwa akitoka kuchezea klabu ya Botofago ya Brazil, ambapo
inaelekea alitundika daluga makusudi kwa kazi hiyo.
Wachambuzi
wengi wa masuala ya soka walikuwa na wasiwasi juu ya uteuzi wake na
iwapo angedumu kwenye kazi hiyo na kweli amefukuzwa baada ya ligi
kumalizika.
Alipoajiriwa AC Milan kama kocha, Seedorf alisema alidhamiria kuirejesha klabu kwenye heshima iliyokuwa nayo awali
AC
Milan walmfukuza Allegri baada ya kufungwa na vibonde Sassuolo 4-3
Januari mwaka huu. AC Milan wamekuwa mabingwa wa Italia mara 18 na
alipofukuzwa walikuwa nafasi ya 11 na wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya
nan echini ya Seedorf.
Chanzo:http://www.tanzaniasports.com/