jaridahuru
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/kitaifa-lowassa-watolea-uvivu-viongozi.html
WANANCHI wa Jimbo la Monduli wilayani Monduli mkoani Arusha wametakiwa kuwang’oa madarakani viongozi wa vijiji wanaoshiriki kinyume na utaratibu kuuza ardhi bila ya kufuata utaratibu kwa kuendekeza zawadi ya bia na nyama choma.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa mara baada ya kuzindua bwawa la maji la Leken lililopo Kijiji cha Selela, Kata ya Selela wilayani Monduli lililobomoka kutokana na mafuriko ya Novemba mwaka 2011 na ukarabati wake kugharimu zaidi ya Sh bilioni 1.1.
Alisema viongozi wa vijiji wanaongoza kwa kuuza ardhi katika Wilaya ya Monduli na kibaya zaidi ardhi hiyo huuzwa kwa wageni kutoka nje ya nchi, wakati mwingine kwa kuhongwa bia na nyama choma.
Alisema wakati umefika kwa wananchi kuwang’oa viongozi wa namna hiyo kwani wanaweza kuingiza jamii ya Monduli katika matatizo makubwa kwa uroho wao binafsi kwani ni aibu kiongozi kwa kijiji kuhongwa bia na nyama choma halafu unatoa ardhi kubwa bila ya kuangalia athari ya baadaye.
Lowassa alisema mkutano mkuu wa kijiji tu ndio wenye mamlaka ya kuuza ardhi kupitia kikao halali na sio kiongozi binafsi hivyo aliwataka wananchi kuwapigia kura ya hapana viongozi wenye kushiriki kuuza ardhi kiholela kwa maslahi yao binafsi.
Alisema kasi ya kuuza ardhi ni kubwa sana hivyo ni lazima kwa kila mkazi wa Wilaya ya Monduli kuwa macho na hilo kwani hali hiyo ikiendelea kutafanya watoto wa Monduli kuwa wakimbizi katika maeneo mengine kitu ambacho ni hatari.
Lowassa ambaye pia amewahi kuwa Waziri Mkuu alisema watu wanaongezeka, lakini ardhi haiongezeki hivyo aliwaasa viongozi wa vijiji jimboni mwake kuacha kuuza ardhi kwa bakshishi ndogo kwani vizazi vijavyo vinaweza kutaabika.
Akizungumzia maji,Lowassa aliwataka wakazi wa Kijiji cha Selela kulilinda bwawa hilo kama mboni ya jicho kwani bwawa hilo lenye uwezo wa kuhifadhi maji yenye lita za ujazo 392,040,000 lina uwezo wa kuhifadhi maji kwa zaidi ya miaka mitatu hivyo ni jukumu la kila mtu kufuata utaratibu wa kulilinda.
Lowassa alisema alipopata ubunge mwaka 1995 tatizo kubwa katika Jimbo la Monduli lilikuwa maji pale Monduli mjini na vijijini ilikuwa tatizo kubwa na wazee wa kijiji cha Selela ndio waliokuwa wakimpa nguvu ya kuwa Mungu atamsaidia na tatizo hilo litafika mwisho na ndio maana kwa sasa Monduli ina maji hadi Kijiji cha Selela chenye wakazi 26,671.
Alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kupeleka fedha za ukarabati mabwawa 6 katika Jimbo la Monduli kiasi cha Sh bilioni 3 likiwemo bwawa la Leken na aliwataka wakazi wa mabwawa hayo kumuenzi Rais kwa kuyatunza kwa faida yao na mifugo.
Related
KITAIFA: PINDA ACHOMOKA KWENYE MADAI YA KESI YA KUVUNJA KATIBA, ALISEMA WANAOKAIDI DOLA WAPIGWE
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana Ijumaa Juni 6, 2014 imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kwa kushirikiana na...
JAMII: MHESHIMIWA JOHN KOMBA MBUNGE CCM APIGA PICHA ZA URODA, ZASAMBAA MTANDAONI, AKANA KUHUSIKA
Picha zinazomwonyesha mh. Captain John Komba zenye mapozi tofauti na mabinti tofauti zimeanza kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania. Kuna picha nyingine nyingi l...
BREAKING NEWZ: GARI AINA YA TOYOTA LANDCRUISER YAPARAMIA MLANGO WA CRDB BANK MOROGORO NA KUINGIA NDANI
Gari limegonga mlango wa kioo wa Benki ya CRDB, mkoani Morogoro. Taarifa zinasema kuwa dereva huyo alikuwa anataka kurudi nyuma kumbe alibonyeza sehemu ya kuendeshea ndo akaishia kuingia CRBD
Post a Comment

:noprob:

:smile:

:shy:

:trope:

:sneered:

:happy:

:escort:

:rapt:

:love:

:heart:

:angry:

:hate:

:sad:

:sigh:

:disappointed:

:cry:

:fear:

:surprise:

:unbelieve:

:shit:

:like:

:dislike:

:clap:

:cuff:

:fist:

:ok:

:file:

:link:

:place:

:contact:
Tabs
Za JuuMitandaoPiga Kura
Za Juu
-
Mmoja wa waasisi wa mtandao wa kijamii wa Instagram, amesema kuwa sheria zake kuhusu picha za uchi hazimbagui mtu yeyote. Kampuni hi...
-
Dar es Salaam. Harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 zimeanza. Polisi wameanza mafunzo yatakayowaongezea uwezo wa kusimamia uchagu...
-
AMA kweli kufa kufaana! Lile bifu zito lililokuwa likitokota kati ya wapendwa wawili, Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu na mwi...









