https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/kitaifa-kampuni-ya-afya-mahakamani-kwa.html
Dar es Salaam. Kampuni ya Indepth Scientific
Company Ltd ya Kenya inayoendesha shughuli zake nchini imeburuzwa
MmSh400 milioni kwa kutumia jina na vyeti vya Mtanzania Kelvin Martin
katika shughuli zake bila ridhaa yake.
Kampuni hiyo inajishughulisha na usambazaji wa
vifaa tiba vya kimaabara vya aina tofauti katika ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati.
Kwa mujibu wa hati ya madai katika kesi hiyo
inayosikilizwa na Jaji Salvatory Bongole, mlalamikaji (Martin)
anailalamikia kampuni hiyo kwa kutumia jina na cheti chake katika
shughuli zake kama ofisa wake mtaalamu mshauri kwa masuala ya maabara,
bila ridhaa yake.
Pia anailalamikia kampuni hiyo kwa kudaiwa kutumia
cheti na jina lake katika kuomba na kujipatia kibali cha kuendesha
shughuli zake kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kupitia Bodi ya
Maabara iliyotolewa bila ridhaa yake.
Mlalamikaji anadai kuwa, mwaka 2009 aliwahi kuomba
kazi kwa mlalamikiwa ambapo aliwasilisha vyeti vyake na kuingia mkataba
wa mwaka mmoja katika nafasi ya meneja masoko, lakini hakuwahi kufanya
kazi badala yake aliondoka na kwenda nje ya nchi.
Hivyo, mlalamikaji anaiomba mahakama itoe amri ya
zuio la kudumu kwa mlalamikiwa na wakala wake kuendesha shughuli zake
kwa kutumia jina na wadhifa wake kwa namna yoyote ile.
Hata hivyo mlalamikiwa katika majibu yake
amekanusha madai yote huku akimtaka mlalamikaji atoe uthibitisho wa
madai yake, anasisitiza kuwa walikubaliana na mlalamikaji