KIMATAIFA: ISIS YACHAPISHA PICHA ZA MAUAJI YA HALAIKI HUKO IRAQ
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/kimataifa-isis-yachapisha-picha-za.html
Vuguvugu la Sunni lenye msimamo mkali la ISIS ambalo
limeteka maeneo ya Kaskazini mwa Iraq limesambaza picha ambazo
zinaonyesha jinsi wapiganaji wake walivyoangamiza idadi kubwa ya
wanajeshi wa Iraq.
Picha zinazosambazwa kupitia internet
zinaonyesha miili ya watu iliyosongamana ndani ya mtaro ikiwa imepelekwa
hapo kwa kutumia malori.
Wapiganaji wa ISIS wanaonekana wakibeba bendera nyeusi ya huku wakichoma miili hiyo na kulazimisha mateka kulala chini
Msemaji wa jeshi nchini mjini Baghdad amesema anaamini kuwa picha hizo ni halali.
BBC haijaweza kuthibitisha uhalali ya picha hizo
kikamilifu lakini iwapo ni za kweli mauaji hayo yatakuwa mojawapo ya
matukio mabaya zaidi kuwahi kuikumba Iraq tangu majeshi ya Marekani
kuingia nchini humo mwaka 2003.
Awali video iliyorekodiwa ilionyesha mamia ya
watu wakilazimishwa kuelekea katika kityuo kimoja huku sauti ikieleza
kuwa ni wanajeshi waliokubali kushindwa.
Duru kutoka vuguvugu la waasi zinasema idadi kubwa ya watu waliotekwa wameuawa.
Mji wa Tikrit ulitekwa na waasi Jumatano wiki iliyopita na majeshi ya Iraq yalikubali kushindwa bila pingamizi.
