JAMII: ASKOFU AWATAKA WATANZANIA KUTOKUBALI KUGOMBANISHWA NA WANASIASA WACHOCHEZI

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/jamii-askofu-awataka-watanzania.html
Watanzania
wametakiwa kutokubali kugombanishwa na wanasiasa ambapo hivi sasa
kumekuwepo na siasa navyama vingi ili kuepuka kuleta vurugu na kuvunja
amani ambayo nchi ya Tanzania imeweza kudumuisha amani na utulivu na
kuwa nchi ya mfano katika bara la Afrika kwa muda wa miaka hamsini
badala yake wawe na msimamo nakuungana kudumisaha amani iliyopo nchini.
Hayo
yalisemwa mapema jana na Askofu mkuu wa makanisa ya International
Evangelism Bw,Eliudi Isangya wakati wa mahafali ya 63 ya chuo cha biblia
kilichopo eneo la sakila wilaya ya Arumeru mkoani Arusha yaliyofanyika
chuoni hapo na zaidi ya wahitimu 79 walihitimu stashahada ya biblia
amabapo ni wanafunzi kumi na moja kutoka nchini Kenya na 68 kutoka
nchini Tanzania ambapo masomo hutolewa bure.
Alisema
kuwa hivi sasa hali ya kisiasa imetawaliwa na ugomvi ugomvi wa mara
kadhaan hali ambayo inahatarisha maisha ya wanaanchi na kuweza kuleta
maendeleo yao badala yake amewataka wanasiasa kufanya siasa za
kistaarabu na tija ili kuweza kuleta maendeleo ya katika majimbo na
taifa kwa ujumla.
Aidha
amewataka waamini wote nchini kuweza kuwa na hofu na mungu ili kuweza
kuenenda vile mungu atavyotaka kwa mapenzi mema na kumtukuza mungu ili
kuwa na amani ili kuweza kuleta maendeleo badala ya kuishi kwa hofu .
Hata
hiyo askofu aliwataka wahitimu hao pamoja na wahubiri kuweza
kuwafundisha watu kuhusu mazingira safi kuanzia rohoni na mazingira
wanamoishi ili kuweza kuepuka vitendo vyote vya kuendana kinyume na
mazingira tunamoishi.
Awali
akisoma risala ya wahitimu wenzake bw. Moses Kaaya alisema kuwa mbali
na juhudi za kupewa masomo ya biblia lakini bado wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali chuoni hapo ikiwemo ukosefu wa miundo mbinu chuoni
hapo ,kukatikakatika kwa umeme hali ambayo inawakwamisha katika
jitihada zao za kujisomea na kuweza kuwa chachu ya mabadiliko katika
jamii ambapo kwa sasa kumekuwepo na kumomomyoka kwa maadili.
Aliongeza
kuwa ukosefu wa maji umekuwa nikikwazo katika eneo hilo la chuo hali
inayolazimu uongozi kufata maji mbali na kuongeza gharama za uendeshaji
na kuomba wizara ya maji kupitia mamlaka ya maji mkoa wa Arusha kuweza
kuwasaidia suala hilo ili kuweza kusoma kwa tija na ufanisi zaidi.
Kaaya
aliongelea suala la uhamiaji haramu ambapo limekuwa tatizo sugu na
kuitaka serikali kuweza kushughulika nalo na kuweza kuepuka machgafuko
yanayoweza kutokea nchini.