https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/afya-singida-kupata-hospitali-ya-rufaa.html
MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko
Vicent Kone amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi 6.7 bilioni kwa
ajili ya kugharamia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoani hapa iliyoko
kijiji cha Madewa nje kidogo ya Singida mjini.
Dk.Kone amesema hospitali hiyo itakapokamilika,itahudumia wagonjwa kutoka mikoa yote ya kanda ya kati.
Mkuu huyo alitoa rai hiyo wakati
akitoa akitoa taarifa yake kwa katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana
aliyetembelea hospitali hiyo hivi karibuni.
Amesema mkoa umetegewa eneo la ekari
283 kwa ajili ya uendelezaji wa mradi wa hospitali hiyo, ambayo itakuwa
ya mfano hapa nchini.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa
wa Singida, Dk Dorothy Gwajima amesema lengo la mradi huo ni kuimarisha
huduma za afya mkoani pamoja na mikoa jirani.
Katibu Mkuu wa CCM akiweka
saini kwenye kitabu cha hospitali ya Rufaa huku Naibu Katibu Mkuu wake
Mwigulu Nchemba na mkuu wa Mkoa wa Singida Kone wakishuhudia.
Dk.Gwajima amesema mradi huo utakapomalizika,utakuwa na majengo 29 yatakayotumika kutoa huduma mbali mbali.
Mganga huyo mkuu,amesema changamoto
inayowakabili ni pamoja na uhaba wa watumishi,nyumba za kuishi watumishi
na ufinyu mdogo wa bajeti ya dawa kutoka bohari kuu ya madawa (MSD).
Kwa upande wake Kinana,alitumia
fursa hiyo kumpongeza Dk.Kone kwa utendaji kazi wake ambao umesaidia
kujengwa kwa hospitali hiyo.
Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Singida (RMO) Bi. Doroth Bwajima akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Amesema baada ya mradi huo kukamilika mkoa wa Singida utaondokana na matatizo ya huduma za afya.
"Ili kumuunga mkono Dk.Kone kwa hili
jambo nzuri la ujenzi wa hospitali ya rufaa ambayo itasaidia Watanzania
wengi kupata huduma ya afya kwa kiwango kizuri,nitahakikisha nina
muunganisha na baadhi ya marafiki zangu wa ndani na nje ya nchi ili
waweze kusaidia kumalizika kwa ujenzi wa hospaitali hii
inayovutia",amesema Kinana.
Mganga mfwawidhi wa hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Dkt Joseph Malunda, akiwaonesha michoro ya
hospitali hiyo viongozi walioambatana na Kinana.
Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakimsikiliza Dkt Malunda.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akisisitiza jambo kwa Kinana.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akimwonyesha Katibu Mkuu kinana
vifaa mbalimbali vilivyopo kwenye hospitali hiyo ya rufaa.
Mbunge MO akiangalia mojawapo ya vifaa vya hospitali ya rufaa ya singida.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini
Mohammed Dewji akisalimiana na Daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama
wa mkoa wa Singida Dkt, Seleman Mutani wakati wa ukaguzi wa hospitali
hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa
akiongozana na mkuu wa Mkoa Kone, Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mh.
Mohammed Dewji, wasaidizi wa Mbunge Duda Mugheny na David Mkufya
wakimwongoza Kinana kutoka nje mara baada ya kukagua hospitali ya Rufaa
ya Mkoa huo