ELIMU: TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO KIDATO CHA TANO KWA TAHASUSI ZA SAYANSI, HISABATI, ENG NA UALIMU MIAKA 3


Katika masomo haya mwanafunzi atasoma masomo ya Sekondari ya Kidato cha V na VI na kufanya mtihani wa taifa wa Kidato cha VI na kuendelea na Mafunzo ya Ualimu kwa mwaka mwingine mmoja ambapo atatunukiwa Stashahada ya Ualimu. Awali, mfumo huu ulikuwa unajulikana kamahalf combination.
Nafasi hizi zinatolewa kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya Sayansi, Hisabati na English katika shule za sekondari nchini.
Masomo tajwa yataendeshwa katika vyuo vifuatavyo: Butimba, Morogoro, Monduli, Korogwe, Songea na Mpwapwa.
Tahasusi zitakazofundishwa ni kama ifuatavyo:
- Chemistry, Biology & ; Education (CBE)
- Biology, English & ; Education (BEE)
- Physics, English & ; Education (PEE)
- Mathematics, English & ; Education (MEE)
- Chemistry, English & ; Education (CEE)
- Chemistry, Mathematics, & ; Education (CME)
- Nutrition, English & ; Education (NEE)
- Agriculture, English & Education (AEE)
- Biology, Nutrition & Education (BNE)
- Chemistry, Nutrition & ; Education (CNE)
- Chemistry, Agriculture & ; Education (CAE)
- Physics, Chemistry & ; Education (PCE)
- Geography, Mathematics, & ; Education (GME)
- Chemistry, Geography & ; Education (CGE)
- Physics, Biology & ; Education (PBE)
- Physics, Mathematics & ; Education (PME)
MAELEZO MUHIMU
(i) Wale ambao tayari wameshatuma maombi yao kwa masomo haya hawahitaji kuomba tena kwani maombi yao yanashugulikiwa.
(ii) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi www.moe.go.tz
OWM-TAMISEMI www.pmoralg.go.tz na NACTE www.nacte.go.tz
(iii) Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
(iv) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM TAMISEMI:www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya Ualimu.
VIAMBATISHO
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu watume maombi yao kwa njia ya Barua ikionyesha anuani kamili ya mwombaji, namba ya simu,pamoja na Nakala ya Cheti cha ufaulu wa Kidato cha IV.
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 10 JULY 2014.
Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)
Kwa wale walioko mikoani, maombi yanaweza kupelekwa kwa Afisa Elimu wa Wilaya ambaye atayawasilisha kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.