BUNGENI: ZITTO AIKALIA KOONI TRA, ATAKA IJIELEZE KWA KUPOTEZA MABILIONI YA WALIPA KODI

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/bungeni-zitto-aikalia-kooni-tra-ataka.html
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kujieleza kwa kushindwa kesi hadi kupoteza Sh340 bilioni za kodi ya ongezeko la mtaji katika uchimbaji urani.
Juni 21, 2014 gazeti hili liliripoti hukumu ya
kesi kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Kampuni ya JSC
Atomredmetzoloto (ARMZ) ikiituhumu kukwepa kodi ya zaidi ya Sh340
bilioni.
Mahakama ya Rufani za kodi ilitupilia mbali madai hayo ikiipa ushindi ARMZ.
Akizungumzia hukumu hiyo, Kabwe ambaye pia ni
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema jana kuwa kukosa kodi hiyo siyo
upungufu wa sheria bali ni uzembe wa Mamlaka ya Mapato na Wizara ya
Nishati na Madini.
“Habari ya Serikali kukosa Sh340 bilioni za kodi
ya ongezeko la mtaji, imenigusa moja kwa moja kwa sababu mbili kubwa,”
alisema na kuongeza:
“Moja, Mwaka 2012 niliwasilisha muswada binafsi
bungeni kurekebisha Muswada wa Fedha 2012 ambao ulikuwa unabadili Sheria
ya Kodi ya Mapato 2004 kwa lengo la kuweka vipengele vitakavyowezesha
nchi kupata kodi kutokana na mauzo ya kampuni za wawekezaji wanapouziana
hisa au mali nje ya nchi.
“Pili, mwaka 2013 niligombana na Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhusu suala la kodi kutoka
Kampuni ya Mantra Resources na Waziri alilihakikishia Bunge kuwa lazima
kodi italipwa. Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo wa TRA, Richard Kayombo
alipoulizwa kwa simu jana alisema asingezungumzia suala hilo Jumapili na
kwamba suala hilo bado lipo mahakamani.