BURUDANI: MAJANGA!! HUSNA NAE ATANGAZA KUWA YUKO TAYARI KUMPA PENZI MWANAUME YEYOTE MWENYE HELA

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/burudani-majanga-husna-nae-atangaza.html
MWIGIZAJI wa kike wa filamu Bongo Husna Chobis ‘Awena’ amesema kuwa
baada kurudi katika biashara zake nje ya nchi yupo tayari kuolewa lakini
kwa mtu mwenye fedha na si mbabaishaji ambaye hawezi hata kumiliki
Bajaji hamuitaji, lakini kwa wale ambao wanaona wanajiweza kuwa
wachapakazi na wanapata fedha ya kubadilisha mboga.
“Kuzaliwa katika familia ya kimaskini ni bahati mbaya, lakini kuchagua mume maskini ni uzembe na haustaili msamaha, ukitembea unajifunza mambo ya mastaa wa Ulaya wanavyoishi wanapotaka kuolewa wanatafuta wanaokwenda nao kimaslahi, hata mimi nahitaji mtu wa kueleweka na kipato pia,”anasema Husna.
Mwigizaji huyo aliyejizolea umaarufu katika filamu za kiasili hasa filamu ya Ndase, anasema moja ya matatizo ya ndoa za kitanzania au kiafrika ni kukosa uchaguzi na kuingia katika uhusiano wa kupotezeana muda kisha kutengana kutokana na kuwa uzembe wa kukosa maamuzi kutoka kwa wanawake wengi.