jaridahuru

Mitandao

BURUDANI: DIAMOND PLUTNUMZ NA KUFURU NYINGINE, AREKODI VIDEO KWA MILIONI 70, VIDEO KUTOKA HIVI KARIBUNI


VIDEO Mpya ya mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz, aliyorekodia London, Uingereza, imemgharimu zaidi ya Sh70 milioni kutayarisha licha ya audio ya wimbo huo kutengenezewa Nigeria miezi miwili iliyopita.
 

Mteule huyo wa tuzo za BET ambaye amemshirikisha mwanamuziki Iyanya kutoka Nigeria katika wimbo huo, amesema video hiyo imemgharimu fedha nyingi, ambazo ameamua kuwekeza katika muziki huku akiamini atavuna fedha nyingi kupitia muziki wake.
 
Diamond anasema anaumia sana pindi anapokuwa akifanya kazi zake kwani huchukua kiasi kikubwa cha fedha na kuwekeza katika muziki ili kukuza bongofleva na kuutangaza muziki wa Tanzania.
 Si kwamba ninafanya hivi kama Diamond, la hasha! Bali ninafanya kwa mapenzi ya Tanzania. Lazima nihakikishe naendelea kuipeperusha bendera ya nchi yangu ili hata wageni wanaonijua sasa waone dogo sikubahatisha. anasema Diamond.
 
Anasema alitumia Dola 25,000 pekee kumlipa prodyuza wa video hiyo, kwani alitakiwa amfuate London yalipo makazi yake.

Related

Habari Mpya 3006389902096237105

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item