AL SHABAAB: MTU ANAE ENDESHA AKAUNTI YA TWITTER YA AL SHABAAB HUKO KENYA AKAMATWA

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/al-shabaab-mtu-anae-endesha-akaunti-ya.html
Maafisa
wa polisi wa Kenya wamemtia nguvuni mshukiwa anayetuhumiwa kuendesha
akaunti ya Twitter ambayo ina uhusiano na kundi la kigaidi la Al shabaab
na uliotoa habari kwamba Al shabaab walihusika kutekeleza mauaji eneo
la Mpeketoni kaunti ya Lamu.
Kwa mujibu wa Ripota wa nguvu kutoka Kenya
Julius Kepkoech, Katibu wa wizara ya Mambo ya ndani na usalama wa taifa,
Mutea Iringo amethibitisha kwamba Ismail Omondi ametiwa nguvuni Tarehe
18 June mwaka huu ambapo hata hivyo Iringo amekanusha kwamba mshukiwa
huyo hana uhusiano wowote na Al Shabaab.
Moja
ya matukio yanayodaiwa kufanywa na Al Shabaab Lamu Kenya ingawa Rais
Uhuru amesema Al Shabaab hajahusika bali hii imekua ikifanywa kisiasa.
Iringo amesema “unaweza kuona kwamba yule anayekiri kuhusika na Alshabaab si mmoja wa kiongozi wa kundi hilo,”.
Inspekta
Jenerali wa Polisi David Kimaiyo awali alisema kupitia ukurasa wake wa
Twitter kwamba “Aliye kizuizini kwa sasa ni mshukiwa anayeendesha
mtandao wa kijamii unaodhaniwa kutumiwa na Al shabaab kukiri kuhusika na
uvamizi”
Hata hivyo Kimaiyo hakutoa taarifa zaidi kuhusiana na washukiwa.
Ismail
Omondi ni mshukiwa wa tatu kutiwa nguvuni kuhusiana na mauaji
yaliyotokea Mpeketoni siku ya Jumapili na Jumatatu ambapo zaidi ya watu
60 wamepoteza maisha.
Mapema
ya siku ya Jumatano, mshukiwa mwingine Ahmed Abdallah anayetuhumiwa
kumiliki gari lililowabeba wavamizi hao alikamatwa huku Salim Dyana naye
akikamatwa na polisi kwa tuhuma za kuliendesha gari lililowabeba
wavamizi kuelekea Mpeketoni Lamu.