KIMATAIFA: PISTORIUS SASA KUPIMWA UCHIZI, WADAI HUENDA ANA UCHIZI

Amri ya jaji inakuja baada ya shahidi mmoja wa upande wa mashitaka kusema kuwa mwanariadha huyo anakumbwa na matatizo ya kuzongwa na mawazo pamoja na kuwa na wasiwasi wakati wote
Bwana Pistorius amekanusha madai ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kusudi
Anasema kwamba kwa bahati mbaya alimpiga risasi kupitia mlango wa choo baada ya kushikwa na wasiwasi akidhani kuwa alikuwa jambazo aliyevamia nyumba yake.