jaridahuru

Mitandao

AJALI: WATANO WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI MBAYA HUKO SEKENKE


WATU watano wamekufa papo hapo na wengine 16 kujeruhiwa baada ya kutokea ajali ya barabarani iliyolihusisha gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace eneo la Mlima Sekenke, wilayani Iramba kwenye Barabara Kuu ya Singida -Mwanza.

Mganga wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, Dk Antony Mbulu, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:30 usiku wakati abiria hao wakienda kwenye sherehe ya Maulid kijiji jirani cha Shelui.
Dk Mbulu aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni dereva Athuman Adam (34) na Ally Wambura (36), wakazi wa Igunga na Amin Salim (45) mkazi wa mjini Singida. Alisema miili ya watu wawili haijatambuliwa.
Kwa mujibu wa Dk Mbulu, ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T547 ASP kushindwa kulimudu kutokana na mwendo kasi.
Alisema kuwa majeruhi watano kati ya 16 waliolazwa kwenye hospitali hiyo, wamehamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa matibabu zaidi huku hali zao zikielezwa kuwa mbaya.

Baadhi ya majeruhi ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema ajali hiyo ilitokana na mwendo kasi na kutokuzingatia sheria za usalama barabarani.
Walidai kuwa ajali ilitokea wakati dereva huyo akipita malori kwa kasi, ndipo akagonga kingo za barabara na kupasua tairi kabla ya kuingia msituni na kupinduka mara nne.
Basi hilo dogo lilikuwa limebeba abiria 21 likitoka mjini Singida kwenda Shelui.

Related

JAMII: BABA ATEMBEA NA MWANAE KWA MIAKA 12..WAAMUA KUFUNGA NDOA

Imezoeleka kuona uhusiano wa karibu kati ya mzazi na mtoto wake lakini si uhusiano wa mapenzi kama ambavyo binti huyu wa miaka 18 ameamua kufanya kwa kuwa na uhusiano na baba yake mzazi na sasa a...

JAMII: JESHI LA POLISI LAWATIA MBARONI PANYA ROAD 36 BAADA YA MATUKIO YA MWAKA MPYA

  JESHI la Polisi nchini linawashikilia vijana 36 wanaotuhumiwa kujihusisha na kikundi cha uhalifu jijini Dar es Salaam, maarufu kama ‘panya road’, ambacho kilizua taharuki kubwa juzi. ...

ESCROW: TRA: WATUMISHI WALIOTAJWA KASHFA YA ESCROW WAKO KAZINI, SEKESEKE LAANZA TENA UPYA

Dar es Salaam. Watumishi wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), waliotajwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow wanaendelea na kazi wakisubiri taratibu za utumishi wa umma kabla ya kuc...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item