KIMATAIFA: MIGOMO AFRIKA KUSINI YASABABISHA KUDUMAA KWA UCHUMI

Bw. Ramatlhodi sasa ameonya kuwa mgomo huo unaupelekeka Uchumi wa Afrijka kusini pabaya,huku sekta ya viwanda na uuzaji nje wa bidhaa za Afrika kusini nazo zikiripotiwa kufifia..
Familia za wachimba migodi pia zimeathirika pakubwa.
Hata hivyo kuna wachache ambao wanataka kurudi kazini, lakini wanahofia maisha yao na wenzao wanaoendelea na mgomo huku kukiripotiwa visa vya mashambulio, na wachimba migodi watano kuuawa katika wiki mbili zilizopita.
Baadhi ya waekezaji wameilaumu serikali ya rais Jacob Zuma kutochukua msimamo thabiti juu ya suala hili.