JAMII: KITOTO CHATUPWA MAENEO YA UDOM..YASEMEKANA BINTI WA CHUO

https://jaridahuru.blogspot.com/2015/01/jamii-kitoto-chatupwa-maeneo-ya.html
Wakati akina mama wengine wanakesha wakimuomba Mungu awabariki na watoto wengine wakikesha kwa sangoma nao wanaomba kupata watoto.
Huyu mdada ameushangaza umma na kuwaacha watu midomo wazi baada ya kujifungua kitoto na kukitupa.
Tukio hilo limetokea maeneo ya chimwaga katika chuo kikuu cha Dodoma maarufu kama (UDOM).
Hata hivyo baadhi ya mashuhuda wanadai kuwa wanahisi huenda kitendo hicho cha kikatili kimefanywa na dada mmoja (jina tunalihifadhi) ambaye alikuwa mja mzito na sasa anaonekana hana uja uzito na akiwa hoi chumbani kwake.
Tulipomfuata na kumhoji alidai kuwa yeye sio mjamzito wala hajawahi kupata ujauzito, na kuhusu afya yake alidai kuwa yuko kwenye hedhi na kama alivyo ada ya kila mdada.