UGANDA: YULE MSICHANA WA KAZI KATILI ALIYEMJERUHI MTOTO HUKO UGANDA APATIKANA NA HATIA..SOMA HUKUMU YAKE HAPA
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/12/uganda-yule-msichana-wa-kazi-katili.html
Yaya wa Uganda ambaye alinaswa kwa kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto mdogo amepatikana na hatia ya ukatili.
Atafikishwa mahakamani tarehe 15 Jumatatu Disemba kupokea hukumu .
Jolly Tumuhirwe aliambia mahakama kuwa alilazimika kufanya kitendo
chake kwa sababu mamake mtoto huyo aliwahi kumchapa mara kadhaa.
Alipokuwa
anaondoka kortini mamake mtoto Angella Mbabazi, alikanausha madai ya
Jolly akisema hajawahi kumgusa Jolly hata wakati mmoja.
Alihoji madai ya Jolly akisema angewezaje kumchapa msichana huyo wa kazi na kisha amuache na mtoto wake?
Awali
tuhuma dhidi ya Jolly kuwa alimtesa mtoto huyo, yalitupiliwa mbali na
mwendesha wa mashitaka wakisema ingekuwa vigumu ,kuweza kuyathibitisha.
Huenda akafungwa jela miaka 5 jela kwa kumchapa na kumjeruhi mtoto.