VYUONI: CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM (DMI) CHAPATA BAHATI YA KUTEMBELEWA NA N/WAZIRI WA UCHUKUZI

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/07/vyuoni-chuo-cha-bahari-dar-es-salaam.html
Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akisaini kitabu cha
wageni katika ofisi ya Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), mara
baaada ya kuwasili chuoni hapo kuangalia shughuli mbalimbali
zinazofanywa na chuo hicho na kuongea na wafanyakazi wa Chuo hicho,
mwanzoni mwa wiki. Kulia kwake anaemtazama ni Kaimu Mkuu wa Chuo hicho,
Kapteni Yasin Songoro.
Mkufunzi
wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), akimpa maelezo ya namna ambavyo
wahandisi wanaofanya kazi ndani ya chumba cha injini ndani ya Meli
wanavyoendesha mitambo hiyo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk.
Charles Tizeba, wakati alipotembea chuoni hapo mwanzoni mwa wiki kuongea
na wafanyakazi wa chuo hicho.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, akimsikilza Kapteni Jumanne
Karume, alipokuwa akimpa maelezo ya namna nahodha anavyoendesha Meli,
wakati alipotembelea Chuo Cha Bahari Dar es Salaam(DMI), mwanzoni mwa
wiki. Kushoto kwa Dk Tizeba ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Kapteni Yasin
Songoro.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (aliyeweka mikono
mfukoni), akimsikiliza Kapteni Peter Mkunja wakati akimpa maelezo ya
namna vyombo vya kujiokoa vinavyotumika endapo meli itazama ama kupata
hitilafu yoyote, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Chuo hicho
Mwanzoni mwa wiki.
Kaimu
Mkuu wa Chuo Cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Kapteni Yasin Songoro,
akitoa maelezo ya namna ambavyo mashine inayotengeneza vipuri
vinayoharibika ndani ya meli inavyofanya kazi kwa Naibu Waziri wa Wizara
ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, alipotembelea Chuoni hapo Mwanzoni mwa
wiki hii.
Sehemu
ya Menejimenti na wafanyakazi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI),
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba
(Hayupo Pichani), wakati alipoongea nao mwanzoni mwa wiki.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)