jaridahuru

Mitandao

KITAIFA: MAALIM SEIF ATAKA MAZUNGUMZO KATIBA MPYA, ASEMA ITAKUWA HASARA KWA TAIFA IWAPO KATIBA MPYA HAITAPATIKANA




Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema Serikali imeshatumia fedha nyingi za wananchi kwenye mchakato wa kuandaa Katiba mpya, hivyo kitendo cha kushindwa kukamilisha mchakato huo kwa wakati, itakuwa ni hasara kubwa kwa taifa.

Amesema kuwa bado serikali ina jukumu la kuhakikisha kuwa katiba mpya inapatikana, ili kuendeza ustawi wa Taifa na kukidhi mahitaji ya wananchi.

Maalim Seif amesema moja ya hatua za kufanikisha kupatikana kwa katiba hiyo ni Serikali kutafuta njia mbadala za mazungumzo, kuhakikisha kuwa mchakato huo unaendelea na unafanikiwa kwa maslahi ya Taifa.

Alitoa kauli hiyo katika Mahojiano Maalum na kituo cha televisheni cha ITV, Dar es Salaam jana. Katika mahojiano hayo, Maalimu Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) Zanzibar, itaendelea kuwepo hata baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kwa vile suala hilo ni la kikatiba na limewekewa misingi maalum. Kiongozi huyo pia alionya kuwa vitendo vya hujuma dhidi ya raia na wageni, vinaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa Zanzibar.

Alisema Zanzibar ambayo imekuwa ikitegemea zaidi sekta ya Utalii, kuendeleza uchumi wake na kukuza pato la taifa, imekuwa ikiguswa na matukio hayo ya hujuma.

Alisema matukio hayo, yanaathiri uchumi, ustawi wa jamii na sifa ya ukarimu kwa Zanzibar. Makamu huyo wa RAis alisema katika kukabiliana na vitendo hivyo, Serikali inatarajia utekeleza mpango wake wa kuweka kamera za CCTV katika maeneo muhimu ya utalii, likiwemo eneo la Mji Mkongwe, ili kuweza kuwabaini kwa urahisi wahusika wanafanya vitendo hivyo.

Kuhusu zao la karafuu kwa maendeleo ya uchumi wa Zanzibar, Maalim Seif alisema serikali imefanikiwa kudhibiti magendo ya karafuu, baada ya kuongeza bei ya zao hilo na kuwashinda wanunuzi wengine wa Afrika Mashariki, ambako karafuu hizo zilikua zikipelekwa.

Alisema katika kuhakikisha kuwa ubora wa karafuu za Zanzibar, unalindwa na kudhibiti wauzaji wengine, Serikali kupitia Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, itaweka nembo maalum “brand”, kuweza kuzitofautisha karafuu za Zanzibar na za maeneo mengine.

Akizungumzia tatizo la dawa za kulevya, Maalim Seif ambaye ofisi yake ndiyo inayohusika na udhibiti wa dawa hizo, alisema bado kuna kazi kubwa ya kudhibiti uingizaji na matumizi ya dawa hizo, kutokana na jiografia ya visiwa vya Zanzibar.

Aliongeza kuwa vita hiyo ni ngumu, kutokana na uwezo mkubwa wa wafanyabiashara wa dawa hizo, ambao wanaweza kuwarubuni watendaji kwa pesa nyingi na kuacha kutekeleza wajibu wao.

Aliongeza kuwa katika kupiga vita dawa hizo, ni lazima kuwepo na ushirikiano na uadilifu miongoni mwa watendaji, hasa wale wanaofanya kazi katika viwanja vya ndege, bandarini na vyombo vya ulinzi.

Related

Kitaifa 6196093949549218911

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item