TANZIA: MAMA ZITTO AFARIKI DUNIA, FAHAMU CHANZO CHA KIFO CHAKE

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/tanzia-mama-zitto-afariki-dunia-fahamu.html
Taarifa za Kusikitisha zimekigubika chumba cha habari cha Jarida Huru, Taifa na Dunia kwa ujumla kwa kuondokewa na mwanaharakati wa wanawake ambae pia ni mama yake mzazi Zitto Kabwe.
Marehemu alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu
Tanzania, (Chawata), Shida Salum, alilazwa katika chumba cha wagonjwa
wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Ami, Masaki, Dar
es Salaam akisumbuliwa na maradhi ya saratani.
Shida ambaye ambae pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Alianza kusumbuliwa na maradhi hayo mapema Agosti mwaka jana
lakini hali yake ilibadilika mapema mwaka huu akiwa mjini Dodoma
akisubiri kuapishwa pamoja na wajumbe wengine wa Bunge Maalumu la
Katiba.
Mheshimiwa Zitto amethibitisha kifo hicho katika 'tweet' yake katika mtandao wa kijamii wa Instagram iliyosema ; "Mama yangu amefariki dunia" na kuomba dua.