jaridahuru

Mitandao

KITAIFA: SERIKALI YAPIGA 'STOP!' MIKUTANO YA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI CCM, NAPE NNAUYE



Mtwara. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ameonja chungu ya uamuzi wa Serikali wa kusitisha mikutano ya hadhara katika mikoa ya Lindi na Mtwara baada ya kushindwa kufungua mashina ya chama hicho mjini Mtwara.
 
Nape ambaye alikuwa mkoani Mtwara kwa ziara ya siku moja, alijikuta akiishia kuwakabidhi bendera za chama hicho viongozi wa matawi ili wakazipandishe wenyewe kimyakimya.
Akizungumzia hatua hiyo, Nape alisema amri hiyo ya kusitisha mikutano imekuwa kikwazo na inadidimiza demokrasia katika mikoa hiyo, hivyo Serikali inapaswa kuibadili ili kuruhusu iendelee kufanyika. Mashina ya chama hicho ambayo yalitarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa wiki ni Shapriya, Coco Beach na Kwajionee.
“Ni kweli ilikuwa twende kuzindua kwenye maeneo yenu lakini… lipo agizo ambalo lilitolewa na Serikali kuzuia mikutano katika mikoa hii, kupitia kwenu ipo haja ya kufungua mikutano ili demokrasia ipanuke zaidi,” alisema Nape na kuongeza:
“Amri hii kwa mtazamo wangu inabaka demokrasia, lazima mikutano iruhusiwe kama hali ni mbaya, kazi ya Serikali ni kulinda huo usalama… nitakwenda kushauriana nao ili mikutano ifunguliwe, sidhani kama masikio yanaweza kuzidi kichwa.”
 

Related

Kitaifa 340854138829579696

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item