KITAIFA: LOWASSA AIBUKA NA MSIMAMO MPYA, AIZUIA JWTZ KUCHUKUA ARDHI YA WANANCHI, AWAPA SIKU 7 TU KUIRUDISHA

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/kitaifa-lowassa-aibuka-na-msimamo-mpya.html
Mbunge wa monduli na waziri mkuu mstaafu. Mhe. Edward Lowassa |
Akizungumza katika uzinduzi wa Bwawa la Migwara lililojengwa upya na kampuni ya Ms Meero Contractors kwa thamani ya Sh870.1 milioni. Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo hilo, alisema wananchi hao wanapaswa kuhamishiwa katika shamba lililokuwa la mwekezaji la Oguru ambalo sasa linamilikiwa na halmashauri.
Alisema sambamba na mifugo yao, wanapaswa kuhamia katika eneo hilo kabla ya mwezi huu, kwani tayari Halmashauri ya Monduli ilishafanya uamuzi wa kuwapa ardhi hiyo zaidi ya miaka miwili iliyopita, lakini suala hilo halijatekelezwa.
“Halmashauri ya Monduli ina madiwani wengi vijana, lakini cha ajabu wanafanya kazi taratibu kama konokono. Tukifanya uamuzi inachukua muda mrefu kutekelezwa, tulishaamua Shamba la Oguru litakaliwa na familia 63 za Nanja na mifugo yao,” alisema Lowassa.
Alisema wakati halmashauri hiyo ikiwa inatekeleza mpango wa kuwanyang’anya wawekezaji mashamba 43 waliyoyatelekeza, yale ambayo tayari yapo mikononi mwa halmashauri wayagawe kwa wananchi.