jaridahuru

Mitandao

KITAIFA: KATIBU CHADEMA NA VIONGOZI WENGINE WA UPINZANI WASHIRIKI MBIO ZA MWENGE WA UHURU


VIONGOZI wa vyama vya upinzani mjini Morogoro, wameshiriki katika Mbio za Mwenge wa Uhuru. Viongozi hao walioshiriki katika mbio hizo ni Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Morogoro, Ngonyani Boniface, Mwenyekiti wa TLP Wilaya ya Morogoro, Juma Kasielo, Mwenyekiti wa Chama cha Jahazi Asilia, Ismail Rashid na Katibu wa UDP Wilaya ya Morogoro, Salum Mwandule.


Viongozi hao kwa pamoja, walipata fursa ya kuushika Mwenge wa Uhuru sambamba na viongozi wengine wa Serikali ya wilaya hiyo na baadhi ya wananchi wa Kata ya Kilakala.


Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Rachel Kassanda, aliwapongeza viongozi hao wa vyama vya upinzani mkoani Morogoro, kwa kutambua umuhimu wao wa kushiriki kikamilifu kwenye mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2014.


Kassanda alitoa pongezi hizo, kabla ya kutoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru katika Kata ya Kilakala katika Manispaa ya Morogoro, juzi. Alisema hayo baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko.


Uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Morogoro ukishirikiana na Manispaa ya Morogoro, ulitoa mwaliko kwa viongozi wa Vyama vya Upinzani ili washiriki mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu.

 
Akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru kwa wananchi katika eneo hilo, Kassanda alisema kuubeza Mwenge wa Uhuru ama kuwatukana waasisi wa taifa hili ni utovu wa nidhamu.
Alisema inapaswa kila mmoja, kulaani na kuwakemea wale wenye tabia hizo.


“Nimeambiwa hapa leo kuna viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani...hili ni jambo zuri kwani Mwenge wa Uhuru ni wa Watanzania wote, bila kujali itikadi ya chama, unatuunganisha sisi Watanzania, bila kujali dini, kabila wala itikadi ya chama...unahubiri amani, upendo na umoja “ alisema Kiongozi huyo.


Aliongeza," Nimefurahi kuwaona viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani kwenye tukio hili...na hii inaonesha juu ya umuhimu wa Mwenge wa Uhuru kwa Watanzania". Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi, viongozi hao waliupongeza uongozi wa Serikali ya Wilaya na Halmashauri ya Manispaa kwa kitendo cha kuwashirikisha kwa kuwapa mwaliko.


“ Tumeletewa mialiko, pia tumepewa usafiri, hili jambo linaonesha Mwenge wa Uhuru hauna chama, ni wa Watanzania wote, nasi tunaungana na wana Manispaa kwenye tukio,” alisema Rashid ambaye ni Mwenyekiti wa Jahazi Asilia.


Kwa upande wake, Ngonyani wa Chadema alisema Chadema haipingi kuwepo kwa mbio za Mwenge wa Uhuru, isipokuwa inahoji juu ya matumizi ya fedha.


“Mimi binafsi sina tatizo na Mwenge wa Uhuru kukimbizwa, ndiyo maana leo (juzi) nipo hapa Kilakala kwenye kata ninayoishi na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kuweka jiwe la msingi la soko,” alisema Katibu huyo wa Chadema wa Mkoa.

Related

Siasa 7973737420060292215

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item