JAMII: WANANCHI WENYE HASIRA KALI WAMCHOMA MOTO MWIZI HADI KUFA USIKU WA LEO G/MBOTO JIJINI DAR

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/jamii-wananchi-wenye-hasira-kali.html
G/MBOTO: Katika kile kilichodaiwa kuwa ni jaribio la kuiba katika kaya moja huko Ulongoni, Gongo la mboto jijini Dar es salaam, Kijana mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja amechomwa moto na wananchi wenye hasira kali hadi kufa akiwa katika jaribio la kutaka kuiba.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa tisa usiku. Hata hivyo inadaiwa kuwa wezi wengine walikimbia na kutokomea bondeni hivyo hawakuweza kufahamika wala kukamatwa.
Polisi walifika katika eneo la tukio na kutoa maiti iliyokuwa imeungua sehemu kubwa za mwili wake.
Picha na Amos Marwa