https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/jamii-msichana-aliyechomwa-na-pasi-sasa.html
NYUMAya pazia! Yule msichana Yusta Lucas (20) mwenyeji wa Mkoa wa
Tabora ambaye alifika jijini Dar kufanya kazi ya u-hausigeli na
kufanyiwa ukatili wa kutisha na bosi wake kisha habari zake kuandikwa,
ametoa siri nzito, Uwazi limemegewa.
Akizungumza kwa uchungu na gazeti hili akiwa wodini kwenye Hospitali
ya Mkoa wa Kitabibu Kinondoni, Mwananyamala jijini Dar, Yusta ambaye
amefanya kazi kwa tajiri yake huyo kwa miaka mitatu alisema:
“Kwanza nataka watu wajue kuwa mwajiri wangu ni binamu yangu,
alinileta hapa Dar kwa ajili ya kumsaidia kazi za ndani pamoja na
kumlelea mwanaye.
“Kipigo hasa kilianza mwanzoni mwa mwaka huu ikiwa ni pamoja na
kuning’ata kwa meno mwili mzima, ndiyo maana mwili wangu wote unaonekana
una mabakamabaka.
“Mateso yangu majirani walikuwa wakiyajua kutokana na kilio changu
lakini walikuwa wanashindwa kunisaidia kwa sababu ya ushirikiano mdogo.
“Kwanza nashangaa sana kwa adhabu yake ya kuning’ata meno mpaka
damu zinabaki kwake. Je, kama nina virusi vya Ukimwi si na yeye
anavipata?
“Sijajua alikuwa anapata wapi ujasiri wa kuning’ata meno. Kwa kweli
nimeteseka kwa muda mrefu sana. Mungu ndiye anajua, lakini nawashukuru
sana majirani walioliona hilo na kuamua kuchukua hatua.”
KUHUSU MAISHA YA TAJIRI WAKE
Aidha, Yusta alianika mienendo mitano ya bosi wake huyo na kusema imekuwa ikimshangaza sana.
MWENENDO WA KWANZA
“Mimi katika kuishi kwangu pale sijawahi kumwona jirani yeyote
amekuja ndani kusalimia wala yeye kwenda kwa jirani kufanya hivyo jambo
ambalo si la kawaida.”
MWENENDO WA PILI
“Yeye (bosi wake) hana mume. Lakini tangu nimeishi pale kwa miaka
mitatu sijawahi kumwona mwanaume ameingia ndani ya nyumba achilia mbali
wanawake wenzake, hata mgeni. Kifupi yeye ni yeye kwa pale nyumbani kama
ana marafiki labda wanakutana mbali.”
MWENENDO WA TATU
“Muda wake wa kurudi nyumbani siku zote ni usiku mnene, amewahi
sana ni saa mbili usiku. Kwa hiyo, muda mwingi mimi ndiyo huwa
nyumbani.”
MWENENDO WA NNE
“Anajiweza, sijui kwa nini aliamua kunifanyia hivi. Maana mtu ana
gari, anaendesha mwenyewe na anasema ana hela, ndiyo maana namshangaa
kuniadhibu kwa kuning’ata kwa meno.”
MWENENDO WA TANO
“Sikumbuki lini nimewahi kumwona akicheka. Muda mwingi anaonekana amekasirika tu kiasi kwamba nimekuwa nikimwogopa siku zote.”
OMBI KWA SERIKALI
Yusta alisema kufuatia matatizo makubwa yaliyompata ameiomba serikali imsaidie aweze kurudi nyumbani kwao Tabora.
SHUKURANI KWA MAJIRANI
Yusta alitoa shukurani kwa majirani waliojitokeza kuokoa maisha yake ambapo alisema kama wasingekuwa wao hajui ingekuwaje.
MANENO YA MUUGUZI
Kwa upande wa hospitali hiyo, muuguzi kiongozi wa zamu siku hiyo,
Mahija Swalehe alikemea tabia za waajiri wa wafanyakazi wa ndani
kuwatesa na kuiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa jicho la tatu
ili kukomesha vitendo hivyo
.
TUJIKUMBUSHE
Yusta alikumbwa na masaibu hayo kwa muda mrefu hadi hivi karibuni
majirani wakiwa na polisi walipovamia nyumba hiyo na kumkamata bosi wake
kisha kumpeleka Kituo cha Polisi cha Oysteraby, Dar ambako anashikiliwa
na yeye kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibu baada ya kukutwa
na majeraha.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camillius Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na