JAMII: MSANII ALIEDAIWA KUPIGA PICHA ZA UTUPU NA MBUNGE, SHAMSA FORD, AKANA KUMJUA MBUNGE HUYO

Picha chafu zinazodaiwa kuwa za star wa filamu nchini Shamsa Ford na mbunge wa Chadema, Salvatory Machemli zimeanza kusambaa kwa kasi mitandaoni tangu jana,. Picha hizo zinawaonyesha wawili hao wakiwa kitandani kwenye mahaba mazito. Hata hivyo picha hizo zinatia shaka kuwa sio halisi ni za kutengenezwa ingawa hatuna uhakika kwa asilimia zote kwasababu msichana anayedaiwa kuwa Shamsa Ford ana umbo tofauti na la star huyo, Shamsa ana umbo la kawaida ki-shape lakini msichana huyo anaonekana kuwa na umbo namba nane.
Jana baada ya kuona picha hizo ambazo zimeenezwa hasa kwenye pages za kisiasa kwenye mitandao ya kijamii zikimuandama mbunge huyo wa ChademaSwahiliworldplanet ilimtafuta Shamsa na kumueleza kila kitu na kwa kujiamini Shamsa alisema sio zake hizo picha zimetengenezwa na pia msichana anayeonekana kiumbo wako tofauti na hata sura na akasema anajiheshimu sana na ana familia yake asingeweza kufanya jambo kama hilo, alipoulizwa je anafahamiana na Mh. Salvatory Machemli pia alikana kujuana nae achilia mbali kuwahi kukutana nae “zimedaiwa kuwa ni mimi but sio mimi, naomba uangalie hizo picha vizuri au kama upo WhatsApp nikutumie halafu uone je ni mimi? kabla sijakujibu” Shamsa alifunguka