jaridahuru

Mitandao

JAMII: MFANYA BIASHARA WA MADINI MJINI ARUSHA ASABABISHA AJALI MBILI KISHA AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI


Mfanyabiashara wa madini, Richard Lucas (29) anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi kichwani baada ya kusababisha ajali mbili tofauti. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema alijipiga risasi juzi saa 12:45 jioni nyumbani kwake eneo la Kimandolu. Alitumia bastola aina ya Luger yenye namba B136986 .
 
 Alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa Lucas alitokea Tengeru akiwa na gari aina ya Toyota Rav 4 yenye namba za usajili T 494 CKY alikokuwa amemfuata rafiki yake aliyekuwa amepata ajali ya kugongwa na gari.

Alipofika eneo la Sekei Darajani, alimgonga mwendesha pikipiki na kuendelea na safari. Mbele kidogo, kwa mujibu wa polisi, aligonga daladala lenye namba za usajili T 636 CUR aina ya Nissan iliyokuwa inachukua abiria. 

Baada ya hapo gari ya Lucas ilipinduka na waliokolewa kwa kupitia dirishani na wananchi.
Inadaiwa alitoka eneo la tukio kwa pikipiki ya kukodi kwenda nyumbani kwao Kimandolu huku akimwacha Vick Mchuma kwenye eneo la tukio.

Alisema baada ya muda, Mchuma ambaye waliongozana naye kwenda kumsaidia rafiki yao aliyepata ajali Tengeru, alipata taarifa kuwa Lucas amejipiga risasi na mwili upo Hospitali ya Mount Meru. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo. 

Wakati huo huo, polisi imetoa taarifa ya kifo cha mpanda mlima, Denis Joeli aliyeuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali chini ya bega la kulia karibu na moyo alipotofautiana na mtu aliyekuwa akimdai Sh 40,000.

Kamanda Sabas alisema tukio hilo ni la juzi saa 8:30 asubuhi kwenye kitongoji cha Olturei-Moivo wilayani Arumeru. 

Alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini Denis alichomwa na Solomon Lembris, waliyetofautiana kauli wakati wakidaiana fedha.

Alisema kuwa baada ya tukio hilo, Lembris alitokomea kusikojulikana juhudi za kumtafuta zinaendelea huku mwili ukiwa umehifadhiwa hospitalini.

Related

GARI LATEKETEA KWA MOTO LIKIWA KWENYE FOLENI JIJINI DAR.

Saa chache zilizopita katika Barabara ya Kawawa, Ilala Dar imetokea ajali ya moto, gari ndogo imewaka moto lakini hakuna mtu aliyeathirika kutokana na tukio hilo. Mmiliki wa gari hilo&nbs...

JAMII: KITOTO CHATUPWA MAENEO YA UDOM..YASEMEKANA BINTI WA CHUO

Wakati akina mama wengine wanakesha wakimuomba Mungu awabariki na watoto wengine wakikesha kwa sangoma nao wanaomba kupata watoto. Huyu mdada ameushangaza umma na kuwaacha watu midomo wazi baada y...

JAMII: UKATILI WAENDELEA KUITESA TANZANIA! AMUUA MKEWE KWA KUMCHOMA VISU HUKO TABORA

Marehemu Zuhura Juma (31) baada ya kuuliwa na mumewe.Na Leah Marco, TABORA/Uwazi  DUNIA inazidi kwenda kubaya! Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Maulid Mussa (35), mkazi wa Kijiji cha Ig...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item