jaridahuru

Mitandao

KITAIFA: MJANE AFANYIWA UKATILI NA SHEMEJI ZAKE KWA KUINGIZIWA MTI MKAVU SEHEMU ZAKE ZA SIRI WAKIMTAKA AHAME

MJANE mmoja (jina linahifadhiwa kwa sababu za maadili) (24) mkazi wa Kijiji cha Omuga, Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara amefanyiwa ukatili wa kutisha wa kusimikwa kijiti sehemu zake za siri na shemeji zake ili kulazimishwa kuhama baada ya mumewe kufariki dunia.

Baba mzazi wa mjane huyo,  Alex Allal aliliambia  gazeti hili kuwa mara baada ya kupata taarifa za ukatili huo aliofanyiwa mwanaye aligundua tayari alishatimuliwa kwake akawa anatangatanga na mtoto wake mdogo wa kiume mwenye miaka saba.

Baba huyo alidai amefedheheshwa na kitendo cha shemeji wa binti yake kwa kumpiga kisha kumfanyia ukatili huo.

MJANEMsichana anayedaiwa kufanyiwa ukatili wa kutisha wa kusimikwa mti sehemu zake za siri na shemeji zake ili kulazimishwa kuhama baada ya mumewe kufariki dunia akionyesha mti uliohusika kwenye tukio hilo

“Baada ya kufanyiwa unyama huo, tuliripoti polisi na kupewa RB namba UTE/RB/256/2014 na mmoja wa shemeji zake aitwaye Isaya Elphas alikamatwa Mei 28, mwa huu na wengine kutoweka,” alisema.

Naye mjane huyo alidai kuwa, alianza kunyanyaswa na shemeji zake hao baada ya mume wake Samwel Elphas kufariki dunia mwaka 2012.

Aliyataja manyanyaso aliyoyapata ni pamoja na kudaiwa kuporwa ardhi ekari mbili zilizokuwa na mashamba ya miwa, migomba, mihogo na mahindi alizoachiwa na marehemu mumewe.
Alidai familia ya wakwe zake imemuomba aondoe shauri hilo katika vyombo vya dola ili wajadiliane na kupata suluhu.

Related

Kitaifa 1536544192469066479

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item