jaridahuru

Mitandao

ELIMU: JK KURUDI KUFUNDISHA TENA, ASEMA YUKO TAYARI KUSHIKA CHAKI

Jakaya-Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa anakusudia kurejea darasani kushika tena chaki kwa kuwa mhadhiri kwenye Chuo cha Taifa cha Ulinzi – National Defence College (NDC) cha Dar Es Salaam.

Rais Kikwete amelieleza hilo mchana wa jana, Ijumaa, Juni 20, 2014, wakati alipotoa Mhadhara (Lecture) kuhusu Usalama wa Taifa (The Security of the Nation) mbele ya wanafunzi wa Chuo hicho kilichoko Kunduchi, Dar Es salaam.

Rais Kikwete amewaambia wanafunzi wa kozi ya pili ya Chuo hicho kutoka nchini na nchi za jirani za Uganda, Kenya na Rwanda: “Najisikia mwenye raha sana kuweza kurudi darasani kutoa mhadhara huu. Tukio hili linanikumbusha enzi zangu katika Chuo cha Kijeshi cha Monduli (TMA). Ni matarajio yangu pia kuwa nitaweza kurudi kuwa mhadhiri katika Chuo hiki baada ya kukamilisha kazi yangu ya sasa.”

Rais Kikwete ambaye alizungumza kwa kiasi cha saa mbili, alianza mhadhara wake baada ya kupata maelezo kuhusu maendeleo ya Chuo hicho na baadaye akajibu maswali ya wanafunzi ambao walimwuuliza kuhusu mambo mbali mbali yanayohusiana na usalama wa nchi.

NDC kilianzishwa rasmi Septemba 2, mwaka 2012 na Chuo hicho kilizinduliwa Rais na Rais Kikwete Septemba 10, mwaka huo huo, 2012 wakati alipotembelea Chuo hicho kwa mara ya kwanza kufuatia juhudi kubwa za uongozi wake kuhakikisha kuwa chuo cha namna hiyo na cha aina yake kinaanzishwa nchini. Rais pia alifungua kozi ya kwanza ya Chuo hicho.

Kundi la wanafunzi wa kwanza kwenye Chuo hicho lilimaliza mafunzo yake Julai 23, mwaka 2013 na sasa chuo hicho kinaendesha kozi ya pili yenye wanafunzi 30. Chuo hicho tayari kimepata usajili kamili wa NECTA ambako kina uwezo wa kutoa shahada ya uzamili katika masomo ya Strategic Studies.

Related

SIASA: "CCM ITASHINDA UCHAGUZI MKUU 2015"-JK AMHAKIKISHIA UHURU WA KENYA

  Taveta, Kenya. Rais Jakaya Kikwete amemweleza Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM), kitashinda katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. Rais Kenyatta kwa upande wake bila ...

TANESCO: MGAO WA UMEME KWA SASA HAUZUILIKI, WATANZANIA WAOMBWA KUWA WAVUMILIVU

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema mgawo wa umeme kwa sasa hauzuiliki nchini kutokana na mabwawa yanayotumika kuzalisha nishati hiyo nchini kukumbwa na ukame. Mkurugenzi ...

TANZIA : MCH. MTIKILA AFARIKI KWA AJALI YA GARI: JINSI ILIVYOTOKEA, R.I.P MTIKILA

Pwani/Dar.  Aliyekuwa Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila (65) amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze wilayani Bagamoyo. Mtikila alifa...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item